Wazazi wawezesheni walimu kiuchumi

Wazazi wawezesheni walimu kiuchumi

Showmax

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2022
Posts
6,592
Reaction score
12,707
Walimu wetu wanatumia mda mwingi Sana kutuandalia kesho ya watoto wetu, vipato vyao havitoshi kumudu mahitaji yao.

Viongozi wa dini wanalishwa na waumini wao lengo kuu Ili wasiwaze watakula nini. Maana huwezi mtumikia Mungu na mali yaani uhudumie kiroho huku ukafanye vibarua Ili familia iishi, thus jukumu la kula ni la waumini.

SAsa kwa walimu wetu wanaotufundishia kesho ya watoto, kwann tusiamaue kutoa kiasi mchango kila mwezi shuleni anaposoma mtoto wako Ili kumpunguzia Mwalimu mzigo wa maisha.

Kuliko awaze kufundisha huku anawaza sambusa zake hazijanunuliwa hii ya kuuza vitu madarasani udhalilisha Sana walimu.

Kama tunaweza wachangia pesa mitume na manabii wa uongo wanaishi kifahari kwann tusiwachangie walimu wetu pia? Mbona ushuru wa taka, ulinzi sijui nini tunalipa? Tuache ubinafsi Watanzania.

Kila mzazi mwenye mwanafunzi awajibike kutoa angalau si chini ya sh elf 2000 ambayo itagawanywa kwa walimu wote wa shule husika kama posho wabakie na wazo moja tu la kufundisha na sio mawazo mengine.

Walimu wanapiga hadi bodaboda, asubui darasani wakitoka shule watoto anakula vichwa hadi Saa nne usiku huyu atajiandaa vipi na masomo ya kesho?

Tuache ubinafsi watz. Elimu bure hii siasa tu na sio hali halisi.
 
Tuwawezeshe Ili wawawezeshe watoto wenu.
 
Unaijua dhana ya ubepari ndugu, tukiwasaidia wao sisi atatusaidia nani, hapa tupu tushawachoka maana kila siku ni michango shuleni na serikali yao inawakataa kwa kusema haitakiwi michango mashuleni
 
Na ni nani atakayewawezesha wazazi kiuchumi ili na wao wawawezeshe waalimu.

Nadhani Hilo ni jukumu la serikali.
 
Na ni nani atakayewawezesha wazazi kiuchumi ili na wao wawawezeshe waalimu.

Nadhani Hilo Ni jukumu la serikali.
Kwani wanaowaweza mitume, manabii, mashehe viongozi wa dini si hawa hawa masikini.

Tuache ubinafsi
 
Back
Top Bottom