JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Zaidi ya asilimia 70 ya wazazi Wilaya ya Mtwara huenda wakakosa haki za watoto wao kutokana na tabia ya kubadilisha majina ya watoto kwenye vyeti vya kuzaliwa, sababu ikitajwa kuwa ni talaka.
Akizungumza Oktoba 31 katika kampeni ya kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa katika Wilaya ya Mtwara inaoyoendeshwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), mkazi wa Magomeni mkoani humo, Zuhura Mrisho amesema kuwa talaka zimekuwa chanzo cha wengi kubadilisha majina ya baba kwenye vyeti vya watoto wao.
“Mwanangu simbadilishi jina hata baba yake akiniacha hata asipojali watoto atabaki kuwa baba tu.
“Nimeachana na mume wangu hataki hata kuwaona watoto, lakini nawasisitiza watoto kuwa yule ndiye baba yao pekee. Acheni kuwabadilishia watoto majina ya baba zao,” amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo, Dunstan Kyobya amesema kuwa wazazi wengi wanakuwa hawana majina sahihi ya watoto wao na kulazimika kubadili mara kwa mara hatua inayowalazimisha kutoa elimu hii.
Amesema kuwa mtoto anatakiwa kuwa na majina sahihi baada ya kuzaliwa ili kuepuka changamoto ya kubadilisha majina.
“Asilimai 70 wanakuja kubadilisha majina ya watoto wao mtoto wakati anaanza darasa la kwanza, akiwa na jina lingine sekondari jina lingine eti limekosewa na chuo lingine.
“Ndio maana tunatoa elimu na kuanzisha kampeni. Tutapita shule kwa shule ili kutoa elimu kwa wananchi wote kwa wingi wa watoto hawa elimu itasambaa zaidi,” amesema Kyobya.
Naye Mratibu wa Vizazi na Vifo Mkoa wa Mtwara, William Felix amesema kuwa wapo wanaokuja kutaka kubadilishha majina hadi ya wazazi wao kwenye vyeti vya kuzaliwa.
“Wengi wanabadilsiha majina yao kwa maana ya herufi wapo wanaotaka kubadilisha ya mama na baba, lakini sheria hairuhusu hata kama wamegombana. Wengi wanakuja na hiyo kesi lakini wakitoa taarifa zao tunawabaini.
“Wengi hawana vyeti ni changamoto wapo wanaotaka kubadili mwaka lakini hatubadili mwaka na siyo utaratibu.
“Wapo wengine wana vyeti lakini wanasema hawana, ukiingiza kwenye mfumo unawakuta yaani majina ya wazazi. Hivyo wyake," amesisitiza Felix.
Chanzo: Mwananchi