Wazazi wenza...!

Hapo kwenye red ndio utaharibu. Nikwambie kitu. Hao watoto as long as mama yao yuko hai kitendo unachosema utafanya hapo kwenye red kisije kikawa na kusudio la kuwafanya wam replace mama yao na mama kambo. Kumbuka hao watoto wanatakiwa wampende mama yao mzazi zaidi ya mama mwingine yeyote. Sasa akihisi unataka kumpokonya pendo la wanawe ndio hapo nae ataleta ushindani. Hata ningekuwa mimi ningewambia wanangu that is not your mother! Nadhani unanielewa kaka yangu.
 
Mimi nadhani watoto ni vema wakae na mama yao uendege kuwatembelea tu. Ni ngumu sana kukaa na amani kama mama wa watoto yuko hai. Lazima atakuwa anakagua wanae wanaishi vipi, mwisho wa siku ugomvi. Mama wa kambo hata akiwapenda hao watoto bado inaweza kuwa shida vile vile. Yaani sisi wamama ukifikiria ulivyoangaika kuwapata hao watoto leo hii wakuone kama mpita njia, lazima ulete shari tu watoto waendelee kuku value kuliko huyo mama kambo.
 
We nawe umezidi uvivu...ndo maana ulifeli vidudu!!Lolz!

hahaha! Ila nimesoma neno baada ya neno.
sijui kwa nini tunapoachika ni ngumu kuukubali ukweli na kumpa uhuru kila mmoja kuendelea na maisha yake.
Suala la kulea watoto wa wengine ni gumu kwa wanawake wengi kwa sababu ya mambo kama hayo. Mama wa watoto anapoanza visa hata kama mama wa kambo alikuwa anawapenda watoto nae anabadilika. Nafikiri hapo muhusika mkuu ni baba kutoruhusu mvurugano wa aina yoyote.
Binafsi mara zingine natamani niolewe na mwanaume ambaye tayari ana watoto. Nahisi kama huwa wana utulivu fulani hivi.
 
Hata wakikaa kwake kama mama ni troublesome matatizo yatakuwepo tu....tena ndo kwanza usumbufu utazidi maana kila saa watoto wamepanda watoto wameshuka kumbe ni usanii tu!
 
Husninyo mara nyingi haya matatizo sio kwamba lazima huo mke wa kwanza awe ameachika... unakuta bado yupo, ila mke mdogo anapokuaja anahakikisha huyo mwenzie anajuta...
 
Hii ni kweli,natumai watakusikia mama
 
Hhahhaahh....ntakununulia pipi aisee!!

Hua sijui wanajisikiaje!!Ila ulivyosema ni kweli...baba ndo anaeweza kuamua kama ageuzwe uwanja wa mpira au la!!Alafu kweli wenye watoto tayari na kama anawajali anakua muda wa kuruka ruka huku na kule hana!!!
 
Husninyo mara nyingi haya matatizo sio kwamba lazima huo mke wa kwanza awe ameachika... unakuta bado yupo, ila mke mdogo anapokuaja anahakikisha huyo mwenzie anajuta...

hilo ni tatizo la wanawake na mabinti wengi kupenda kuonekana yupo juu zaidi ya mwenzio.
Linapokuja suala la bi mdogo na bi mkubwa nahisi litanishinda. Nataka kuwa peke yangu.lol.
 
Inategemea. Nina jirani yangu ana watoto kama wanne wa nje. Wengine alizaa kaba hajaoa, wengine akiwa na mkewe. Akizaa wakifika miaka minne hivi anawaleta ndani.

Mkewe anawatesa kweli kweli na mumewe wala hajali.
Kuna wanawake wanapenda wame zao wakizaa watoto wawalete ndani wakiamini kuwa wakiwahacha kwa mzazi mwenzie basi kuna possibility kubwa ya kukumbushiana, na kuongeza mwingine.

Kuwa na watoto hakumpunguzii mwanaume muda wa kuruka kwa sababu wababa mambo ya kulea si kazi yao kwa hiyo hata kama ana watoto kumi; muda anao wa kutosha tu what matters ni tabia ya mtu.

Hhahhaahh....ntakununulia pipi aisee!!

Hua sijui wanajisikiaje!!Ila ulivyosema ni kweli...baba ndo anaeweza kuamua kama ageuzwe uwanja wa mpira au la!!Alafu kweli wenye watoto tayari na kama anawajali anakua muda wa kuruka ruka huku na kule hana!!!
 
Alafu kweli wenye watoto tayari anakua muda wa kuruka ruka huku na kule hana!!!
umeona eeh! Hawa masharo akikuoa we umejifungua unalea mtoto mwenzio wa pembeni analea mimba. Too bad kwakweli.
Niletee pipi yangu nilale huku nakula.
 
Hahahhaha....NK nisamehe kwa kucheka ila hapo pa naenda kumuona mtoto alafu anakumbushia pameniacha hoi.Tatizo la huyo mwanaume ni kwamba hajatulia na wala hajali wanawe hata chembe...alafu kama hiyo haitoshi kakutana na mwanamke asie na huruma!!Pole yao hao watoto....
 
hilo ni tatizo la wanawake na mabinti wengi kupenda kuonekana yupo juu zaidi ya mwenzio.
Linapokuja suala la bi mdogo na bi mkubwa nahisi litanishinda. Nataka kuwa peke yangu.lol.

Mpenzi nani asiyependa kua peke yake.... sometimes inabidi ku blame wanaume wenyewe...
 
Hao kama wameza pita huo mtihani ni gurantee kua NO kuachana... inapendeza..
 
hiyo ipo kweli ila kuna wale ambao walizaa halafu wakapitia kipindi kigumu na hao waliozaa nao hadi kufikia hatua ya kususiwa watoto; huwa ni watulivu, ngumu kurudia makosa labda kama ukiolewa nae wewe ndio uanze madoido ndani ya nyumba.
 
Mpenzi nani asiyependa kua peke yake.... sometimes inabidi ku blame wanaume wenyewe...

bora afanyie huko huko akirudi nidhamu iwepo kuliko kuleta ndani tuwe wawili. Lol.
 
hiyo ipo kweli ila kuna wale ambao walizaa halafu wakapitia kipindi kigumu na hao waliozaa nao hadi kufikia hatua ya kususiwa watoto; huwa ni watulivu, ngumu kurudia makosa labda kama ukiolewa nae wewe ndio uanze madoido ndani ya nyumba.

Wengine wanakuwa hawana mdomo tatizo ni waliowatangulia!
 
Mpenzi nani asiyependa kua peke yake.... sometimes inabidi ku blame wanaume wenyewe...

Ila ni ngumu kujua na kukubali kumshea mtu....binafsi siwezi maana nadhani ni mchoyo sana kwa kitu nnachokipenda!
 
Haya mambo ni kumtanguliza Mungu. Maana unaweza kukaa na mtoto wa mwenzio (kama mama kambo). Mumeo akawa anampenda mwanae, which is natural, wewe ukaanza kuona wivu. Yaani kuna ile hali ya kuona image ya mwanamke mwenzio mlio share penzi la mume wenu (hata kama it is history) through the kid. Yaani ni rahisi kumpenda adopted kid kuliko mtoto wa mumeo. Sijuhi kwa nini.

Na hii si kwa wanawake tu hata wanaume. Tumesikia story ngapi wanaume wanaua watoto wa wake zao, iwe ulaya au afrika ni same. Nadhani ni human nature, so ni kusali tu tupewe moyo wa upendo.
 
ila ni ngumu kujua na kukubali kumshea mtu....binafsi siwezi maana nadhani ni mchoyo sana kwa kitu nnachokipenda!

kumbe we mchoyo....lol
sasa mbona unanishauri nisiwe mchoyo na mimi?
What if unakutana na mtu ambaye polygamy ndio lifestyle?????????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…