Wazazi wetu:-Mgeni akiwa anakula ukimuangalia unapigwa, ukipigwa ukalia unapigwa na usipolia unapigwa

G4N

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
4,283
Reaction score
9,925
Wazazi wetu walikuwa hawaeleweki wanataka nini.

*Mgeni akifika halafu mtoto akawa anamuangalia, anapigwa.
*Akiwa anakwepa kumuangalia mgeni (anaangalia chini), anapigwa.

*Mgeni akitengewa chakula halafu mtoto akamuangalia wakati anakula, anapigwa.
*Mtoto akipigwa akalia, anapigwa.
*Na akipigwa asipolia, anapigwa.

Sasa sijui walitaka mtoto afenyeje?

Lkn hivi Sasa hawa akina junior, wanalia halafu mzazi anageuka kuwa mtumwa kumbembeleza.
 
Nakumbuka nilivyokuwa mdogo, kuna watu walikuwa wanakuja pale nyumbani kusali na mama(walikuwa na kikundi flani hivi)

Sasa siku moja walikuja usiku tumepika wali nyama, walishtukiza tu sio kawaida yao

Wakati mama anawapakulia nikapeleka kiherehere changu huko jikoni nikaropoka 'sasa mboga itatosha kweli?'

Aisee klichofuata siwezi sahau. Hadi mwiko ulihusika....
 
Mimi nilishawah katwa na ule upawa wa kupakulia mboga wa chuma kwenye goti kisa kiherehere cha kupambania wageni wasipewe na soda zetu .
 
Hii yote ni umaskini

Familia haijazoea kuona soda na vijuice vipo vipo tu home

Nilijaribu siku kuwa nanunua soda naweka ndani nikisema zitakuwa zinanywewa kidogo kidogo , mbona ziliisha siku hiyo hiyo..

Wakiingia wakitoka wanatoka na soda
 
Wazazi wetu walikuwa hawaeleweki wanataka nini.

*Mgeni akifika halafu mtoto akawa anamuangalia, anapigwa.
*Akiwa anakwepa kumuangalia mgeni (anaangalia chini), anapigwa.

*Mgeni akitengewa chakula halafu mtoto akamuangalia wakati anakula, anapigwa.
*Mtoto akipigwa akalia, anapigwa.
*Na akipigwa asipolia, anapigwa.

Sasa sijui walitaka mtoto afenyeje?

Lkn hivi Sasa hawa akina junior, wanalia halafu mzazi anageuka kuwa mtumwa kumbembeleza.
mtindo wa malezi imabadilika sana...

mfano,
wakati naishi nyumba za kupanga jirani yangu moja alikua na mtoto wa kiume anasoma chekechea....

sasa yule mtoto akirudi kutoka shule mama yake alimzoesha kumkagua alichofundishwa siku hiyo huko shuleni. Na mtoto nae, alizoea hali hiyo, na kwahivyo alikua akimsomea mama yake picha, michoro ya wanyama na vitu mbalimbali walivyo fundishwa huko shuleni, kwa ufasaha sana, na daima mama alifurahi na mtoto alifurahia sana malezi na upendo wa mama yake elimu 🐒

Tatizo sasa,
Baba yake akirudi, na kumuita mtoto yule kwaajili ya ukaguzi ule ule kama aloufanya mama yake, nadhani yule mtoto huwa anajawa woga, hasira iliyojaa kiburi, mithili ya nyoka mweusi aliebugudhiwa 🐒

ndugu zangu mtoto hua anavibreti kwa kilio kile cha hasira na sauti ya kujizuia huku akitetemeka kama kiswaswadu.

akiambiwa soma hiki ni nini, au hii picha ni ya nini, mtoto hugoma kabisa... ni kilio na kutetemeka tu.....

unajua kwanini anafanya hivyo,
anajua akisoma kwa kukosea, atapigwa na akisoma kwa usahihi atapigwa tu vilevile 🐒

kwahivyo amechagua best option ni kukaa kimya apigwe tu yaishe.
sasa ndio malezi gani hayo 🐒

Tuwalee watoto wetu kwa upendo ndrugo zango 🐒
 
Mgeni akija ukamuomba Hela ,unapigwa

Mgeni akija usipo msalimia ,unapigwa

Ukipigwa ukawa haulii ,unapigwa maana unaonekana sugu [emoji23]

Chakula kikitengwa mezani ukaanza kunawa kabla ya wakubwa ...unapigwa

Mgeni akija ukaanza kumlilia uondoke nae ..Unapigwa

Chakula kikitengwa kuna bakuri la baba ,huwa ndio kuna mapaja na nyama nyingi ,ole wako ukaweke mkono huko ...kichapo mpaka baba mwenyewe akupe[emoji23]

Baba akija nyumbani akakuta umekaa kiboya sebuleni ..unapigwa Bila hata sababu..

Ukitumwa dukani ukachelewa ..fimbo ..

Kwenye kabati huwa kuna vyombo vya kutumia siku wageni wakija tu ,siku mama akikuta unatumia hizo sahani au vikombe wakati Hakuna mgeni ..utapigwa fimbo na ngumi juu ,usipokimbia shauri yako

Hawa watoto WA siku hizi wanapelekwa hadi Shule aiseee ...Sisi tunaenda Shule wenyewe na njia tunayopita asubuhi kuna mbwa hatari ,kama huna mbio imekula kwako..na Hakuna njia nyingine [emoji28]
 
Jamani😂😂😂
 
Mama angu akiwa anakusema ukimjibu anasema una dharau, ukikaa Kimya anasema una kiburi., ukiondoka anasema unajifanya umekua..
Sijui hua anatakaga nifanye nini😏😏
Watoto wa 2000 kweli mlikua mna raha , unakosea unasemwa tu , bi nkubwa alishanirushia panga nikalikwepa likaenda kukata mgomba .
 
Hapo anakusema wakati mwiko ushakukatikia mguuni😂😂😂.. Ila wazazi hawa basi tu yani..
 
Haya ndio malezi yetu ya kiafrica , huku kwa wenzetu litoto lina waambia wazazi eti limeamua kuwa shoga na wazazi wanalichekea tu.
 
Kuna malezi ndyo lakini wazazi wetu walizidi aisee😂
 
waafrica bila hivyo ni hatari, ebu fikiria tu mimi nikiwa kadgo kabisa kwenye michezo ya kibaba na kimama ,namwekea pilipili kwa papuchi katoto ka kike ,ili nione itatokea nini ? Apo lazima upigwe kama punda .
 
Back
Top Bottom