Wazazi wetu wana hofu juu ya utekaji, inasikitisha sana

Wazazi wetu wana hofu juu ya utekaji, inasikitisha sana

DON YRN

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2019
Posts
665
Reaction score
1,572
Wasalaam!,

Nimekaa wiki 1 nzima sijawasiliana na wazazi wangu nikipambana na purukushani na namna ya kulipa hili deni la mama yetu.
Leo napokea simu ya baba yangu, baada ya salamu mzee ananambia, nanukuu; "Mwanangu, usiwe unakaa muda mrefu bila kutupigia simu tukajua unaendeleaje maana tuna hofu kwa sasa ya watu kutekwa na wasirudi tena"

Hii kauli imenifikirisha sana, ina maana watekaji na wasiojulikana wametengeneza hofu kiasi hiki kwa watanzania na wala watawala wetu hawashtuki suala hili lilivyo serious?.

Inasikitisha sana kwamba vijana tulio kwenye utafutaji hatujui kama leo au kesho tutarejea nyumbani tukiwa salama au lah!

$ham3 on you Watekaji kwa kusabisha hofu kwa Watanzania.
 
Mliambiwa juzi msiwalazimishe kufanya vingine. Sijui kama kauli ile pale Mwz uliielewa ?!.
 
Back
Top Bottom