Toa sababu na si kupinga tu bila sababu. Kuna vigezo vinavyotumika vya uanzishwaji mkoa mpya na si kuamua tu. Kwa kumjibu wa mwongozo wa TAMISEMI wa mwaka 2014, vigezo vya kuzingatia katika kuanzisha mkoa ni pamoja na kuwa na ukubwa wa eneo lenye kilomita za mraba usiopungua 20,000. Pia kuwa na wilaya nne, idadi ya watu isiyopungua asilimia tatu ya idadi ya kitaifa, tarafa zisizopungua 15, idadi ya kata zisizopungua 45 na idadi ya vijiji visiopungua 150. Mkoa mpya wa Chato utakuwa na tarafa 18, kata 87, vijiji 360 huku ukiwa na ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 30,215, lenye watu zaidi ya milioni moja laki tano.