GE2025 Wazee Dodoma waombwa kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura Oktoba

GE2025 Wazee Dodoma waombwa kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura Oktoba

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewataka wazee wa mkoa huo kuhamasisha jamii kujitokeza kupiga kura Oktoba 29, 2025, na kuhakikisha vijana wanalinda amani ya nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewataka wazee wa mkoa huo kuhamasisha jamii kujitok.jpg
Amesema wazee wanayo nafasi kubwa katika kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo, akibainisha kuwa Dodoma ya sasa imebadilika na kuwa mji wa kuvutia kutokana na jitihada za Serikali.

Aidha, Senyamule amesema Serikali inaendelea kutoa elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa ili kuimarisha afya za wazee.

Wazee hao wametumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuboresha huduma za afya na miundombinu, huku Mkuu wa Mkoa akiahidi kushughulikia changamoto hizo na kuhakikisha wazee wanapewa kipaumbele siku ya kupiga kura.
 
Back
Top Bottom