Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,898
- 40,547
Jana Des 2, 2025 saa 7:11 mchana Watanzania wote wameona na Dunia imeshuhudia mliosilimishwa/kubatizwa na kupewa jina la Wazee wa Dsm mkipiga makofi kushangilia kauli ya mama Samia aliposema nguvu iliyotumika kukabiliana na Vijana Oct 29 ilikuwa ya kutosha.
Tumeona mlivyotumia vizuri posho mliyolipwa kuhudhuria na kwenda kushangilia vifo vya Watanzania wasio na hatua wengine wakiwa wameuawa ndani ya seble za nyumba zào.
Jana mmeshangilia vifo vya mama Ntilie waliopigwa risasi wakiwa wamejifungia kwenye vibanda vyao, mmeshangilia vifo vya Wanafunzi waliokuwa wanarudi nyumbani toka vyuoni, mmeshangilia vifo vya waandishi wa habari waliouawa wakiwa kazini kama Master Tindwa, mmeshangilia Mauaji ya Shehe Majini aliyeuawa akiwa kwake.
Kiujumla mmetuonyesha ushetani wenu badala ya utu, tumeshahudia uhalisia wenu.
Asanteni.