Wazee na wanamichezo njooni tulizungumzie hili kidogo

Wazee na wanamichezo njooni tulizungumzie hili kidogo

Source07

Senior Member
Joined
Oct 5, 2018
Posts
196
Reaction score
353
Heshima kwenu wapenzi wafatiliaji wamichezo na wanamichezo kwa ujumla!

Moja kwa Moja niende kwenye hoja yangu.

Hivi karibuni kama wiki3 zilizopita tulishuhudia kuona uliyokua uwanja wa Taifa ukibadilishwa jina kwa ajili ya kumuenzi Hayati BMW kwa Amri ya Mh. Rais hivyo uwanja huo ukaitwa Benjamin Mkapa Stadium! Sawa haina tatizo kabsa ila sasa nilichokita tukijadili hapa nihiki nilichokisoma kwenye mitandao yakijamii haswa page za Wasafi wakitangaza show za wasanii wao zitakazo fanyika Kahama, katika maelezo yao wanasema uwanja wa Kahama ndio uwanja wa Taifa. Kahama National Stadium, yaani hadhi uliyokua nao uwanja wa Taifa kabla kubadilishwa jina leo hadhi imepewa uwanja wa Kahama. Sawa hakuna neno ila, je Kahama stadium ina kidhi vigezo vyakuitwa Uwanja wa Taifa?

Nakama hili ndio mbona TFF hakuutangaza huu uwanja kua ndio uwanja wetu wataifa kwa sasa, au hata serikali kupitia waizara ya Michezo mbona hawauutangaza uwanja huu kua ni waTaifa? Hawa Wasafi wametoa wapi mandate ya kuita huu uwanja wakahama kua ndio NATIONAL STADIUM!

Ifahamike kua uwanja kuitwa au kuwa ni uwanja wa Taifa ina maana kua mechi zetu zote zitakazo kua zinajumuisha mechi za mataifa mengine haswa zile zilizo kwenye calendar ya FIFA zitachezwa hapo, so wanataka kusema sasa tutakua tunaishuhudia Taifa Stars akicheza Kahama, kucheza huko haina shida ila, je Kahama stadium ina hadhi kweli yakuitwa KAHAMA NATIONAL STADIUM?

Na kingine toka ule uwanja umebadilishwa jina kweli hadhi yake imeshuka Sana kiasi yakwamba husikii Tena ukiitwa uwanja wa Taifa kwanini? Je, kuubadilisha jina ndio kumeathiri mpaka hadhi ya ule uwanja uliyokua nayo hapo mwanzo? Kuna shida gani tukauita Benjamini Mkapa National Stadium? Kuna shida gani, maana sasa hata ukiingia getini unakuta tu jina ni BENJAMIN MKAPA STADIUM au ndio kusema kubadilishwa kwa jina ndio kumeathiri moja kwa moja kuitwa uwanja wa Taifa?

Nimelileta kwenu hili wadau tulijadili kwa mapana sana, au labda nimimi uwelewa wangu mdogo naamini humu wapo manguli watanisahihisha!

Naomba kuwasilisha!
 
Kweli Kahama kuna uwanja unaitwa wa Taifa na hata show yake mwaka juzi alifanyia pale. Somethin must be done soon.
 
Kweli kuna vitu tunavipuuzia sana na nivyamsingi mno!
Hizo ni Nick names tu jamani, ukienda kwenye majina rasmi yanayotambuliwa huwezi kukuta hivyo.
Dar Live inaitwa Uwanja wa Taifa wa Burudani hapo napo je?
Kuna Msaniii anaitwa Major Kunta..., afande Selle, nk Vip hapo napo tuwaite akina Kamanda Mabeyo na Sirro tujadili.
Kuna huyo anaitwa Prof.Jay hapo napo tuwaite TCU tujadili amepataje uprofesa?
Anyway majina ya ziada ya Utani yasikuchanganye Mkuu weee Piga kazi tuu.
 
Hizo ni Nick names tu jamani, ukienda kwenye majina rasmi yanayotambuliwa huwezi kukuta hivyo.
Dar Live inaitwa Uwanja wa Taifa wa Burudani hapo napo je?
Kuna Msaniii anaitwa Major Kunta..., afande Selle, nk Vip hapo napo tuwaite akina Kamanda Mabeyo na Sirro tujadili.
Kuna huyo anaitwa Prof.Jay hapo napo tuwaite TCU tujadili amepataje uprofesa?
Anyway majina ya ziada ya Utani yasikuchanganye Mkuu weee Piga kazi tuu.
So Kahama stadium nickname yake ndio KAHAMA NATIONAL STADIUM afadhali umenipa somo umenifunua ufahamu sikua nalijua hili..barikiwa mkuu
 
Back
Top Bottom