kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Mzee Yusuph Makamba alipewa nafasi ya kuzungumza kwenye mkutano huo alisema kama kweli wote waliosimama na kumsifia Dkt. Samia Suluhu wameongea wakimaanisha basi wasimame na kupitisha azimio la kuwa Samia Suluhu ndiye atakua mgombea pekee kwa mwaka 2025.
"Naona kila mmoja akisimama hapa anasema 2025 ni Dkt. Samia. Sasa kama sio wanafki tupitishe maazimio leo hapa hapa kuwa hakuna mgombea mwengine CCM ni Dk. Samia, hapo hata wale wanaoumezea mate urais wataacha.” Mzee Makamba.
Aidha Mzee Makamba akaongelewa suala la watu Kumsifia Rais na Kusema anaupiga mwingi
"Kama mnataka mumchague mtu lazima mumsifu watu wajue ana sifa, kwahiyo hata wale wanaopinga tukisema umeupiga mwingi ni nahau, nina shemeji yangu pale ana tatizo na kuupiga mwingi, kuupiga mwingi maana yake ni mtu aliyefanya kazi nyingi na kubwa."Mzee Makamba.
"Wapinzani hoja zao ni mbili, katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, mama yangu kule kijijni hawezi kushiba katiba, kwanza ukimwambia kuhusu katiba atakujibu ni kitu gani" Yusuf Makamba, Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM