Wazee wa gambe, ili ulewe kabisa unakua umetumia pesa kiasi gani?

Wazee wa gambe, ili ulewe kabisa unakua umetumia pesa kiasi gani?

Leo nimeamka nikajiuliza hili swali. Maisha hayako fair kabisa, kuna mwingine buku 5 tu tayari analewa, na kabla ya kuzuia viroba buku tu ilitosha kufanya mtu apate starehe hio.

Kwa upande wangu ukiniona nimelewa ujue imekatika kuanzia laki 3, na hapo nikiwa sina kampan kabisa. Ikitokea nipo chimbo wanalouza vinywaji kwa bei za VIP inaweza fika hata 500k+

Na huwa situmii bia kabisa, ni liquors na liqeurs tu.

Je wewe hadi ulewe unakua umezika kiasi gani?
Laki 3 inaondoka ukiwa huna kampani,sijui labda hata viwanja unavokwenda navyo vinachangia.Kwa maana kama unakunywa bia hizi za 2,500 ina maana utakuwa umekunywa bia 120,sasa kama hulewi hapo kuna shida mahali...
 
Back
Top Bottom