Wazee wa Jumuiya ya Ahmadiyya wakutana Dar kujadili changamoto za maadili na amani

Wazee wa Jumuiya ya Ahmadiyya wakutana Dar kujadili changamoto za maadili na amani

DodomaTZ

Member
Joined
May 20, 2022
Posts
84
Reaction score
118
1.png
Viongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya Kusini kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara wamekutana Nchini Tanzani katika Semina ya siku mbili (Aprili 20 na 21, 2024) Nchini Tanzania na kushirikisha washiriki 120 kutoka Nchi 15.

Semina hiyo imefanyia Jijini Dar es Salaam na mada kubwa iliyowakutanisha viongozi hao ni kujadilia suala la maadili katika nchi zilizoalikwa kushiriki.

Walioshiriki ni viongozi wenye umri wa miaka 40 na zaidi, semina ikiwa ni maelekezo ya Khalifa Mkuu ambaye anaishi Uingereza akiwa pia ametuma wawakilishi wake wawili ambao ndio waendeshaji wa Semina husika.

Mbali na maadili, mambo mengine yanayojadiliwa ni nafasi ya Wazee katika Jamii, masuala ya dini Pamoja na kuzorota kwa usalama Duniani na haja ya ushirikiano wa Kikanda na kimataifa.
3.png
Baadhi ya Nchi zinazoshiriki ni Tanzania, Cameroon, Malawi, Uingereza, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kenya, DR Congo, Uganda, Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini na Burundi.

Kaidi Majlis Ansarullah Tanzania Ahmadiyya, Dkt. Swaleh Pazi amesema "Dunia ya sasa inakabiliana na vita ambavyo vinahitaji mchango mkubwa wa viongozi wa dini, ili kusonga mbele.

"Majanga kadhaa yanaripotiwa katika maeneo tofauti Duniani, ikiwemo kuzuka kwa vita vinavyosababisha hofu kubwa ya kiusalama, ongezeko la mmomonyoko wa maadili na kuvurugika kwa mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Nchi na nchi.

“Uelewa wa washiriki utaimarishwa ili kuwawezesha kutekeleza kwa ufanisi majukumu yao ya kiroho katika kutumikia ubinadamu na kuboresha usalama wa Dunia na kuifanya iwe mahali bora pa kuishi.

"Hakuna nafasi ya kuabudu kwa usahihi mahali isiyokuwa na amani. Mizozo inayoendelea Mashariki ya Kati ingeweza kutatuliwa kwa urahisi ikiwa meza ya majadiliano ingetumika.
2.png

Mwakilishi kutoka Uingereza, Abdul Khaleque Talukdar

"Tuko hapa kuweka na kuimarisha njia za kudumisha amani, ili kutuwezesha kuhubiri dini zetu kwa urahisi, kutoa elimu kwa watu wetu na kuweka mipango mingine ambayo itawanufaisha binadamu."

Aidha, ameeleza kuwa semina hiyo itatoa mapendekezo na mikakati ya utekelezaji kwa viongozi katika nchi husika ili jumuiya hiyo ifikie lengo linalokusudiwa na kuwa msisitizo utawekwa katika kuimarisha malezi katika ngazi ya familia.

Ameongeza: “Tunatambua juhudi za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kupambana na mmomonyoko wa maadili nchini, lakini viongozi wa dini wana jukumu kubwa la kuzidisha juhudi hizo katika ngazi ya familia ili kujenga taifa bora."

Upande wa Mwakilishi kutoka makao makuu ya Jumuiya hiyo Nchini Uingereza, Abdul Talukdar, amesema: "Hivi karibuni tulifanya mkutano wa amani London, Uingereza, ambao ulionyesha ni nini kinapaswa kufanywa. Hii ni kwa sababu dini zote zinahubiri amani, ili Dunia ipate usalama uliokusudiwa."

Mshiriki kutoka Kenya, Abdulaziz Gakuria amesema: “Maendeleo ya teknolojia, hasa uwepo wa Mitandao ya Kijamii, yameharibu malezi ya Watoto. Mambo kadhaa yameibuka ikiwemo ndoa za jinsia moja, ushoga na usagaji, jambo linahitaji mchango mkubwa wa wazee katika kurejesha maadili katika nchi zetu.”

Pia soma: Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania: Haki za Binadamu zinapozingatiwa amani inaendelea kustawi katika Jamii zetu
 
Mnisamehe tu,ila nikionaga viongozi wa dini hii naonaga ni viongozi wa ugaidi na wasababishi wa mateso na maumivu mengi wa wanadamu wenzao,hii dini ni laana kwa ulimwengu.
 
Back
Top Bottom