Mzee baba ukimwi nilipimwa jana hiyo hiyo baada ya dokta kuniambia itabidi tupime vyote mpaka ukimwi ili kama unao uanze dozi mapema kabla hujachelew nami nikakubali bila hofu mpaka dokta akaniuliza je umewahi kupima? Nikamwambia hapana alishangaa imekuwaje nimekuwa jasiri kiasi kile kuliko wengine wakiambiwa wapimwe na ukimwi kama hawakuwahi kupima hukataa vikali.
Hata mimi nilijishangaa imekuwaje nimekubali bila hofu ya kukutwa ninao na Mungu ni mkubwa kipimo cha HIV kikaja negative wala sikuonesha kushtuka akili yangu nilishaishet pale pale kuwa napima kama ninavyopima malaria tu na hata nikikutwa ninao nitasurvuve fresh tu maana ukimwi haubadili mfumo wa mwili kama ilivyo kansa, kisukari na presha… maana hayo magonjwa yanakubadili kabisa mzee ila ukipata ukimwi unakula kitimoto kama kawaida, unakunywa bia kama kawaida, unakula mapilau mawali na maugali kama kawaida tena ukiupata unaambiwa na dokta ongezea ka kula matunda na mazoezibkwa wingi so why niuogope ukimwi mzee.
Yaani katika magonjwa ambayo siyaogopi hata kidogo ukimwi unashika nafasi ya kwanza.
Kwa hiyo mzeebaba nikijijenga kisaukolojia namna huyo wakati napima na mambo yakawa safi na hata sasa baada ya miezi mitatu nitaenda kupima tena mimi mwenyewe.