Wazee wa magari mtandaoni hasa hasa BEFOWARD

Wazee wa magari mtandaoni hasa hasa BEFOWARD

Ukikijua kikokotoo Cha TRA kilivyo hauwezi hangaika na hizo Bei hapo. Inshort sijaona bongo gari ya chini ya 9M Hadi liingie road
Ni kwa wakati huu ambao USD iko juu. Miaka 6 nyuma wakati ule USD 1 ni Tsh 1700, hadi 7mil unaweka gari barabarani. Kuna mtu aliagiza na kuweka Nissan March kwa milioni 4. Hapo kalipa kila kitu. Hizo bei hapo zitakuwa ni FOB tu.
 
Habari mkuu
Msaada,
Ukichagua Option ya CIF & Clearing kwenye website ya Beforward
Maana yake gari imejumuisha (CIF, Agency fee & Port charges)?

Unachotakiwa kulipia hapa Tanzania ni KODI YA TRA TU iliyoko kwenye kikokotoo(System calculator)?

Msaada Tafadhali.
 
Umeshindwa kumwambia kawaida mpka umuite mshamba? Kweli stress za bongo c mchezo
Chief ni kumvungia tu, akili yake ndio ilipoishia hapo, mtandaoni ni jalalani, kuna timamu, kuna wenye utindio wa ubongo, kuna wenye akili timamu, kuna chenga, wangese wapo, kila namna, na wote hao lazima tuwapokee kwa mikono miwili..

Tuheshimu tu mawazo yake, kwamba kafikiri wee, akili yake imeishia hapo kwenye "MSHAMBA"
 
Huu utaratibu kwa TRA ni wa toka nyuma, yaani wanakuchapa kodi ya ukweli.

Na ukisema ufanye appeal, gari linakuwa na storage charges zina pileup, maana linakuwa bandarini muda huo (wiki moja ndo muda usio na storage charge). Na appeal zinachukua muda kusort out.
Ukitaka ufanye appeal unaomba gari ipelekwe kwenye bonded ware house huko charge ni $100 kwa mwezi
 
Mwenyewe mwezi mzima huu nimetafuta Premio F ya 2003/2004 at least chini ya 70,000Km kwa $3000 hakuna huko Beforward.

Nimejaribu kuwasiliana nao Bf Tz wanitumie link kama ninaweza pata gari hii ninayoitaka nao wameikosa labda $3800+ tena siyo nyingi.

Cha ajabu ukipitia pages za waagizaji wa ndani wanaagiza gari hiyo tena utakuta 54,000KM kwa 13M-15M ilhali kwa Beforward hata kwa bei yao hiyo hupati.

Je hawa wenzetu huagiza kutoka mitandao ipi huko Japan?

Je hizo KM zao ni za kuaminika kweli au ni ile michezo ya yard ya kushusha KM?
Hayo magari yenye low km hua wameshusha km za hayo magari na ukisema unayanunua hua hawakupi TBS inspection kwenye file la gari
 
Ukitaka ufanye appeal unaomba gari ipelekwe kwenye bonded ware house huko charge ni $100 kwa mwezi

Ooh, sikuwahi kujua kama unaweza kuchagua hii option ya bonded warehouse.

Pia inabidi kuwa na Clearing Agent mwenye uelewa mzuri, wengine wamekariri vitu hata logics hawana.
 
Habari mkuu
Msaada,
Ukichagua Option ya CIF & Clearing kwenye website ya Beforward
Maana yake gari imejumuisha (CIF, Agency fee & Port charges)?

Unachotakiwa kulipia hapa Tanzania ni KODI YA TRA TU iliyoko kwenye kikokotoo(System calculator)?

Msaada Tafadhali.
Hapana.

Utalipia gharama ya gari na nauli ya kuileta (CIF) utalipa gharama za bandarini na wharfage. Gharama za kuitoa bandarini ndio ambazo hutalipa maana umeshazilipa wakati unanunua gari.
 
Kwa wale mnaotaka kuagiza magari-Stay informed CIF zimebadilika msije kujikuta katika wakati mgumu
Reference Number:20213098418
Make:TOYOTA
Model:IST - NCP 60/61/65
Body Type:HATCHBACK
Year of Manufacture:2003
Country:JAPAN
Fuel Type:PETROL
Engine Capacity:1001 - 1500 CC
Customs Value CIF (USD):2,360.33
Import Duty (USD):590.08
Excise Duty (USD):147.52
Excise Duty due to Age (USD):885.13
VAT (USD):760.95
Custom Processing Fee (USD):14.16
Railway Dev Levy (USD):35.41
Total Import Taxes (USD):2,433.25
Total Import Taxes (TSHS):5,618,685.08
Vehicle Registration Fee (TSHS):450,000.00
TOTAL TAXES (TSHS):6,068,685.08
 
Ooh, sikuwahi kujua kama unaweza kuchagua hii option ya bonded warehouse.

Pia inabidi kuwa na Clearing Agent mwenye uelewa mzuri, wengine wamekariri vitu hata logics hawana.
Ila inatakiwa uombe mapema kwa kumuandikia kamishna kabla gari haijafika
 
Tatizo serikali zetu sijui nani kapanga makodi makubwa kiasi iko... Gari japan bei kitonga kwetu ni juu...

TRA wapitie tena huu ujinga wao na kuurekebisha
Kama sahizi kodi sio rafiki tu ila watu wanaendesha DWD huko road je kodi ikiwa million 1 si itakuwa foleni inaanzia getini kwako mpaka posta
 
Back
Top Bottom