Wazee wa Mathematics: Jibu lipi ni sahihi hapa?

Wazee wa Mathematics: Jibu lipi ni sahihi hapa?

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
4,134
Reaction score
10,644
Kuna scientific calculator na Calculator ya simu.

Zote zimepewa hesabu inayofanana lakini majibu yako tofauti!
FB_IMG_1661702809309.jpg
 
Kwa bodmas jibu ni 9

Ilichofanya scientific calculator 2(2+1) imekifanya ni mabano yote.. So imefungua kwanza ndio maana jibu limekuja 1

Mfano ukichukua
6÷2(x+y)

Step inayofata itakuwa ni
6/(2x+2y)

X ikiwa 2 na y 1
Jibu ndio linakuwa ni 1
 
Acha ujuaji
B bracket- fanya chochote ndani ya bracket
O open bracket
D divide
M multiply
A add
S subtract

So;
B 2+1=3
O 3*2=6
D 6/6=1


Hapa hatupimani nani anajua zaidi bali ni suala la kuelimishana tu kwani hakuna anayejua kika kitu isipokuwa Mungu tu.

Haya hebu tuanze darasa:-

6÷2(2+1), hii ni sawa na kuandika, 6÷2×(2+1), kwa sheria ya MAGAZIJUTO (forget about BODMAS), lazima tuanze na expression iliyomo ndani ya mabano "MA" yaani (2+1) ambapo unapata 3, hivyo expression nzima inakuwa hivi; 6÷2×3; katika expression hiyo kuna matendo mawili; tendo la kugawanya na kuzidisha, kwa sherai ya MAGAZIJUTO ni LAZIMA uanze na kugawanya ndipo umalizie na kuzidisha kwani MA= Mabano, GA=Gawanya, ZI=Zidisha, JU=Jumlisha, TO=Toa, kwahiyo 6÷2×3 ni sawa na (6÷2)×3,

Yaani, 6÷2×3=(6÷2)×3= 3×3=9.

Kama unayohoja hapo karibu tujadiliane kwani kujadilana ni moja ya njia ya kujifunza, ni kitu ambacho wenzetu Wazungu hufanya na hivyo kujiongezea elimu, tofauti kwa sisi Waafrika ni mashindano ya nani anajua zaidi hatimaye siku zote tupo nyuma ya Wazungu.
 
Kwa bodmas jibu ni 9

Ilichofanya scientific calculator 2(2+1) imekifanya ni mabano yote.. So imefungua kwanza ndio maana jibu limekuja 1

Mfano ukichukua
6÷2(x+y)

Step inayofata itakuwa ni
6/(2x+2y)

X ikiwa 2 na y 1
Jibu ndio linakuwa ni 1
Hivi kwa akili zako za kawaida 6 ikigawanya hizo namba jibu linakuja 9...hesabu hazina ujanja hapo jibu ni moja hakuna cha kwa bodmas jibu 9
 
Hapa hatupimani nani anajua zaidi bali ni suala la kuelimishana tu kwani hakuna anayejua kika kitu isipokuwa Mungu tu...
Mkuu na wew na akili zako unaona kabisa jibu la 9 ni sahihi wakati ni kubwa kuliko inayogawanya ambayo ni 6 hafu mbna huyo jamaa kuelezea vizuri tu ni basi tu umejaza fuvu.

Ok nitajitie kirefu cha BODMAS na acha na MAGAZIJUTO maana ni sisi tumetohoa usahihi wake upo kwenye neno BODMAS
 
Back
Top Bottom