Wazee wa Mathematics: Jibu lipi ni sahihi hapa?

Wazee wa Mathematics: Jibu lipi ni sahihi hapa?

Hii hesabu hamjakubaliana jibu mpaka leo wana JF wataalam wa hisabati?
 
Hapa hatupimani nani anajua zaidi bali ni suala la kuelimishana tu kwani hakuna anayejua kika kitu isipokuwa Mungu tu.

Haya hebu tuanze darasa:-

6÷2(2+1), hii ni sawa na kuandika, 6÷2×(2+1), kwa sheria ya MAGAZIJUTO (forget about BODMAS), lazima tuanze na expression iliyomo ndani ya mabano "MA" yaani (2+1) ambapo unapata 3, hivyo expression nzima inakuwa hivi; 6÷2×3; katika expression hiyo kuna matendo mawili; tendo la kugawanya na kuzidisha, kwa sherai ya MAGAZIJUTO ni LAZIMA uanze na kugawanya ndipo umalizie na kuzidisha kwani MA= Mabano, GA=Gawanya, ZI=Zidisha, JU=Jumlisha, TO=Toa, kwahiyo 6÷2×3 ni sawa na (6÷2)×3,

Yaani, 6÷2×3=(6÷2)×3= 3×3=9.

Kama unayohoja hapo karibu tujadiliane kwani kujadilana ni moja ya njia ya kujifunza, ni kitu ambacho wenzetu Wazungu hufanya na hivyo kujiongezea elimu, tofauti kwa sisi Waafrika ni mashindano ya nani anajua zaidi hatimaye siku zote tupo nyuma ya Wazungu.
Uko sawa boss
 
Bila vitendo tutahangaika sana. Pitia na piga kura hapa

 
Back
Top Bottom