Wazee wa Mila Wilayani Serengeti, Mkoani Mara, wametoa onyo kali kwa Kijana yeyote atakayeshiriki maandamano, wakisema atatalaniwa na kutengwa na koo yake
Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Angelina Marco, Wazee hao wamesema Wananchi wa Serengeti wanategemea shughuli za Kilimo na kutafuta kipato cha kujikimu, hivyo hawako tayari kufungiwa ndani kutokana na fujo za Vijana.
Wamesisitiza kuwa endapo Serikali haitachukua hatua, wao kama Wazee watasimama kulinda amani ya eneo hilo.
“Hakuna utaratibu unaofuatwa kwenye haya maandamano; wengi wanafanya fujo. Sisi tulidai uhuru kwa mkoloni bila kutumia panga wala mishale, tulitumia maneno na tukaupata. Sasa hawa wanataka nini katika nchi yao? Serikali ipo, kuna utaratibu wa kuwasilisha changamoto. Acheni haya. Vijana, fanyeni kazi zenu kwenye nchi huru, msiingizwe kwenye makelele yasiyo na maana,” alisema Mzee wa Mila
Aidha, Wazee hao wameeleza kuwa Serikali haikatazi maandamano, bali utaratibu uliotumika katika matukio ya hivi karibuni haukufuata misingi na haustahili kuigwa kama sehemu ya utamaduni wa maandamano.
Katika kikao hicho ambacho pia kilihusisha viongozi wa Bodaboda na Wazee wa Mila, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Angelina Marco, amewahakikishia wananchi kuwa hakuna zuio lolote la shughuli Serengeti na kwamba wananchi wataendelea na maisha yao kama kawaida.