Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Sawa.
 
Somo jipya hili
 
Mkuu kuna mazingira mtu anakusababishia ajali na cha kukulipa hana....labda umtoe uhai..

Mimi nilishawahi kugongwa na daadala nyuma, kupambana na dereva ni katoto hakana leseni, daladala halina bima, kumsachi mfukoni ana elfu 50 tu, nikazichukua nikaenda kutengeneza gari kwa 250,000/....ila niliachana nae kiroho safi kwa sabau maisha ya barabarani bado yanaendelea......Sasa mtu kama huyo ningesema tuaze mambo ya polisi, ingekuwaje unadhani..?

Tanzania ibaki tu hivi hivi..
 
Mkuu hizi ni theories za Ulaya, Canada na USA...

Kibongo bongo ajali nje nje ukishakuwa ni mtu wa barabarani kila saa haijalishi unaendesha PASSO AU NISSAN FUGA..

Mashimo barabarani, punda anakatiza barabara, bodaboda, mikokoteni, mabasi yapo rafu sana, malori,...mara mvua inyeshe barabara zikatike...
Mikokoteni barabarani, Walevi wanaendesha barabarani, magari mabovu kibao ambayo muda wowote yanakusababishia ajali..... Western countries hawana haya mambo kama sisi..

Ulaya,USA, Canada uendeshaji wake hauwezi kufanana na bongo hata kidogo..
 
Kwa niaba ya mleta Uzi
Niwapongeze wachangiaji wote hasa wale waliojikita zaidi kwenye vitu vya kujengana na kuelimishana na kuburudishana pia..

Uzi hauna hata mwezi lakini coments tayari zipo 2k...Uzi wa tarehe 15/12/2020..

Ni moja ya uzi kwa upande wa JF garage unaosisimua na kukimbia sana..

Tuchangie bila kugombana..
 
Makampuni ya bima unakomaa nao wanakulipa.

Kuna gari iligongwa na canter tena ikiwa mpya kabisa. Uzuri wa hilo canter lilikuwa na bima third party.

Ila ile kampuni ya bima ikataka kukwepa, ila walikomaliwa mpaka wakatengeneza gari.

Hawa usiwalazie damu.
 
Na mimi niwashukuru wachangiaji wote kwa kuuendeleza.
 
Ha ha ha kuna uzi kwanini magari bongo yanachakaa haraka...ukijua kuna hayo uliyoyataja utajua kwanini gari hazichukui round zinachakaa.
 
Hata traffic wanafanya makosa sana wanapokuja kupima ajali.

Wengi wanakwambia mmalizane kiuhalisia ni kazi ya bima.

Mimi nikikwangua mtu, bima italipa. Siumizi kichwa.
 
Kuna ukubwa wa makampuni yanaruhusiwa kukata bima za ndege.

Bima za ndege zote nadhani zinakatiwa bima UK au SA.

Kibongo bongo hakuna kampuni yenye uwezo wa kukata bima za vyombo hivyo.
 
Zebra zebra .. fine yake huwa inauma kinoma 😃😃😃 nilishapigwa mkeka wa zebra roho iliuma kishenzi .. alafu trafic mwehu tu maana hakukuwa na watu, ila nilipo mkazia akanilima
 
Evolving thread.

Insurance, Road Trip, Services, Garages, Rants.

No specific topic.

I like this thread.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…