Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Hela ya zebra inauma sana mkuu.. wakati mwingine unakuta hakuna watu, au kuna mtu mmoja nae hata hasomeki kama anataka kuvuka au lah.. mie kwa mfano issue ilikuwa ni kunyooka tu, pasipo kuangalia pande zote kama kuna mtu anataka kupita
Hapo alikuonea. Zebra unasimama kama kuna mtu anataka kuvuka.
 
Wa huku dar naona kwa sasa malori na mabasi ya morogoro road yanawatosha.
Hawafuatilii vibao vya 30, na Mungu awaongoze waendelee hivyo hivyo.
Siku wakiamua kimara-kibaha, mwenge-morocco, kilwa road yani ni vichwa tu
 
Road trip yangu ilikuwa Dar - Moro, wakati wa Moro - Dar nilirudi na bus.

Nilikuwa na sister, mzigo ulikuwa ni Athlete. I enjoyed the trip.... Crown tamu aisee ile comfortability yake si mchezo, yan sometimes inavutwa mpaka anavuka 140 lakini nafeel kama bado yuko kwa 80. Sis angu akiwa barabarani ni anadrive kama mwanaume, hanaga wasiwasi na traffic kabisa.

Another trip was Dar to Arusha na Kidia one. Ilikuwa Poa kiasi, Shekilango tulitoka 06:00 kufikia saa kumi na dk 29 tulikuwa around Tengeru. Napenda ile view ya Wami, Tanga ile milima, na wapi pale kunakuwaga na mashamba kibao ya katani, Mombo nk
 
Hongera mchuchu
 
Duh leo nimetenda dhambi roho imeniuma sana. Nilikuwa na gari sijaizoe. Taa ya mafuta imewaka range inanionesha nina km20 tu. Nikaamua niweke mafuta ya kunifikisha home tu nikaweka 10,000 nilijua itaongeza range hadi km60 hivi. Baada ya kuweka mshale haukusogea wala range haikubadilika. Nikaenda ninapoenda range inashuka.
Kurudi nikapita njia ile ile range iko 14, nikapita pale kituo cha mafuta nikamwambia Yule dada nimeweka mafuta hapa kwako lakini gauge haikupanda wala kuonesha kuna mafuta yameingia, umeniibia! Dada Yule akasema sijakuibia nimekuwekea hela ulionipa nikamwambia haiwezekani kusiwe na mabadiliko kwenye gauge, ikabidi niende kituo kingine nikaweka 10, aisee gauge ikakurupuka ikapanda sana na range ikaja kwenye 110km. Hapo nikajua ni kweli aliweka mafuta nimemsingizia tu. Nimejisikia vibaya sana.
 
Nimegundua wanawake umri wa kati mnapenda sana Crown!
 
Uchawi ndo unaanzia hapa
 
Naomba siku nikusababishie ili janga [emoji38]

ila faini ya seat belt inazungumzika mbona, ukiikubali we mzembe unless uwe umekutana na traffic kichomi
Itanibidi nitembee na kamba ya kukufunga kabisaa...Ili ukivua seat belt lamba ibaki..[emoji28][emoji28][emoji28]

unakuta ni majira ya saa saba mchana, asakri akiangalia salio alilotumwa na bosi halijajaa,walahi hakuaachii...

Sasa hivi askari wakali sana maswala ya seat belt kwa anaweza akakagua magari kumi asiambulie kitu, akikuta seat belt haijatumika, anabonyeza hapo hapo..
 
..please weka pic ya sister hapa tumpe credits zake...[emoji28][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…