Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

mimi nikifunga mkanda ndo najiona nipo vizuri, nisipofunga najiona naelea kwenye kiti.
Belt ya abiria ina taa yake, inablink kwa sifa kwa hiyo nafanyaga kuwaonesha hiyo taa tu
Crown ipo, vits new model ipo tena inapiga alarm vibaya mno.

Hawa kina Ist twende kazi tu, belt itafungwa ukiona traffic kwa mbali
 
Hapo alikuonea. Zebra unasimama kama kuna mtu anataka kuvuka.
Alijua akifika nitaanza kulia, au nitakimbilia kumpa ya kiwi, huwa naziweka hela pale mbele mda mwingi huwa nakuwa mwenyewe nadra sana kunikuta na mtu kwenye gari, alipofika nikashusha kioo, akawa anatazama zile huku anacheka cheka, akazunguka gari akarudi namtazama tu 😀😀😀.. ndio akaanzisha hilo.. nikamuambia sawa andika tu, nikampa leseni .. akaandika bado anajichekesha huyo nikasepa.. ila roho iliniuma sana.. nilijua ananione kabisa na sikutaka ligi nae
 
Hiyo hutokea chief... ukiweke wese mshare kama haupandi au zile km. Unaizima kwanza gari. Mie imeisha nitokea hiyo.. na ndicho nilichofanya
 
Binafsi niseme tu kifupi-Speed ni hatari sana kwetu sisi sote.Ajali zinaongoza kwa kutumaliza sisi vijana kila kukisha bila sababu za msingi.Binafsi naamini kama advisable speed sehemu nyingi duniani ni kati ya 80-100kph,basi ni matokeo ya tafiti mbalimbali juu ya usalama wa driving na ikapendekezwa hvyo.Bora tuchezee hapa kuwalinda na wengineo.
 
Tandale ni mfano mmojawapo wa kutuonyesha kwamba reckless driving is dangerous.
 
Nafurahia komentsi tu.
Nikionaga picha zako kule selfika nakumbuka enzi zangu napuyanga kwenye Motoways! Nilikula ban miezi 6 nilipita kwenye construction zone yenye limit 50mph. Mimi nilipita na 100mph(makosa mawili hapa kwasababu speed limit ni 70mph). Ilikuwa north huko sikumbuki ni M ngapi ila ilikuwa natoka M6 Birminngham on my way to catch M56 naelekea Manchester. Nilikutana na bahasha ya kaki baada ya siku tatu, aidha nikubali kuwa ni mimi nilikuwa naendesha au niende mahakamani kujitete, nilikubali nikapigwa hio ban na faini £200.
 
Wala nisiwe muongo,ni ngumu sana kwangu kuendesha gari chini ya 140kph, labda kwenye limit nafuata ili limit ikiisha Mungu anilinde tu.
 
Dahhh,ukiona bahasha la kaki tu unawaza bill au fine mzee Baba.
 
Seat belt ni lazima ukipanda gari langu.

Hata ukikaa seat ya nyuma ntahakikisha umefunga belt ndo naondoa chombo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…