Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,092
- 53,496
Ilishawahi nitokea kama hii.Duh leo nimetenda dhambi roho imeniuma sana. Nilikuwa na gari sijaizoe. Taa ya mafuta imewaka range inanionesha nina km20 tu. Nikaamua niweke mafuta ya kunifikisha home tu nikaweka 10,000 nilijua itaongeza range hadi km60 hivi. Baada ya kuweka mshale haukusogea wala range haikubadilika. Nikaenda ninapoenda range inashuka.
Kurudi nikapita njia ile ile range iko 14, nikapita pale kituo cha mafuta nikamwambia Yule dada nimeweka mafuta hapa kwako lakini gauge haikupanda wala kuonesha kuna mafuta yameingia, umeniibia! Dada Yule akasema sijakuibia nimekuwekea hela ulionipa nikamwambia haiwezekani kusiwe na mabadiliko kwenye gauge, ikabidi niende kituo kingine nikaweka 10, aisee gauge ikakurupuka ikapanda sana na range ikaja kwenye 110km. Hapo nikajua ni kweli aliweka mafuta nimemsingizia tu. Nimejisikia vibaya sana.
Gari ilikuwa harrier tako la nyani ya mshkaji.
Niliweka mafuta kama ya 50K. Nikajua gauge itapanda mbeleni.
Namrudishia gari akalalamika nimerudisha bila mafuta. Ikabidi nimrushie 50 ingine aweke. Akaenda kuweka mzigo ukaruka mpaka full.
Akajisikia vibaya kinoma. Akataka kurudisha mpunga, nikamwambia akaushe.