Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Mwamba kakaza hakuna kuchimba dawa anawahi destination.

Ila he is right. Stops zinachelewesha sana. Mi huwa naplan stops kabisa hakuna kusimama hovyo.

Nikiwaza nna km700+ to cover every minute counts
 
Tunatakiwa tuwe na uzi wa Tanzania's best tarmac roads na worst tarmac roads.

The worst naona ni Shinyanga - Mwanza via Misungwi. Yani ina matuta yasiyo na rasta za taarifa wala mabango. Uko umeiva tuta hii hapa! PAMBANA! Potholes usiseme afu mihandaki mikubwa na haikwepeki imejaa through all lanes.

Nilikuwa napelekeana moto USIKU na mwamba mmoja ana Kluger juzi... yeye anayafukia tu at 110+ kmph, niko nyuma yake namtumia kama pacemaker na guide wa matuta yalipo kwa kuangalia udundaji wa suspension yake

Tuta moja mwamba kalivaa nikaona suspension yake haijacheza sana acha na mimi niliingie... *****!!! Gari ilipiga vibaya mno. From that moment nikakubali mkubwa mpishe nikamwacha aende salama nikanyoosha mikono ku surrender. Nakagua gari leo naona stabilizer link imekatika [emoji23][emoji23] Nimepata adabu na mimi


Ndio yale mambo ya "you can go fast but I can go anywhere"
 
Hiyo barabara mbaya sana.
 
Kuna mshkaji wangu chapombe alikata kamba kwa ulevi wa safari.

Njiani wamekula mzinga akiwa chakari. Madokta wakasema huduma ya kwanza ni detox ndo mengine yakafwata.

Akakata roho huku anafanyiwa detox.

Toka siku hiyo nikimpa mtu lift utabeba maji ya kunywa na soda au juisi tu. Labda mambo ya kulakula.
 
Adventure napenda tukiwa convoy ya magari mengi tunaofahamiana.

Na nimeshafanya hivyo na huwa nafurahi sana.

Ila nikiwa peke angu kusimama hovyo najiona kama mchawi.

Imagine unasimama pale Same sijui unajinyoosha hata wanaokupita wataona huyu jamaa amechanganyikiwa.

Ila endapo nitasimama sehemu za kula, ndo nakaa sana. Hata saa nzima nakaa tu.

Nikichomoka hapo nazima gari nyumbani nimeshaipaki.
 
Mwamba kakaza hakuna kuchimba dawa anawahi destination.

Ila he is right. Stops zinachelewesha sana. Mi huwa naplan stops kabisa hakuna kusimama hovyo.

Nikiwaza nna km700+ to cover every minute counts
Hata mafuta siongezi njiani.

Labda niwe natembea zaidi ya km 800.

Chini ya hapo full tank nikijaza pale total mcity siku naondoka. Inatosha mpaka ninapofika.

Mengine najaza destination.

Kusimama hovyo kunaudhi sana.

Naweza endesha 700km non stop. Nahakikisha nimebeba carton ya maji ya kilimanjaro na buble gum za PK zile za mint kama pakti 20 hivi.
 
Segera-Chalinze.

Chalinze-Mbezi.

Hizo barabara unaweza pasua rim.

Barabara za Arusha mjini zote ni takataka. Hasa ile ya kuanzia mnara wa saa kunyoosha mpaka kiwanja cha ndege kisongo.
 
Wese kutosha ni jambo moja, kuna mwingine anapenda gauge ikisoma half tank tu ajazie tena. Gauge iwe inapepea kama bendera full time

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Duh hukojoi? Una bladder ya cc2500 au
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…