Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,092
- 53,496
Kuna jamaa mwingine anaendesha Dar express ile ya Nairobi.Jana nlikua Safari na BM Coach(VIP's & Private Seaters), Dereva ana kovu kwenye paji la uso mixer Upara na Pete ya Ndoa ya gold. Plate namba ni DPF(Namba naihifadhi). Yaani huwezi amini kila nikibook BM nakutana na huyu Dereva. Sasa nnachotaka kusema hapa ni kwamba kuna watu tukubali wana vipaji vya kuendesha magari na wengine tunaiga au kulazimisha fani.
Huyu Mwamba ni Shida. Kwanza sijawahi kumuona kakamatwa alafu safari zake zote iwe route ya Dodoma, Moro au Moshi~Arusha ni mwendo wa speed 40 to 48km/h. Anazingatia Vigezo na Masharti ile ile na anatembelea Manual. Salute kwake.
Haijalishi mtafika saa ngapi lakini mwamba anakazia humomhumo na anajali muda huyo Khataree, kuna Njemba iliomba kushuka kuchimba dawa sehemu isiyo rasmi, dereva akampa Chupa kubwa lile la Lita 2 akamwambia ajiongeze. Nikazidi kumuelewa.
Aafu, kuna Bi Mkubwa juzi kati alivurugwa akapayuka anataka nyimbo za Dini kwenye gari eti hapendi kuona viuno vya wadada wa BongoFlavour wakiwa nusu Uchi Mwamba akamute Sauti kisha tukatembea kama masaa 4 hivi bila Volume kisha akaichia ilivyofika kwenye sinema. Bi Mkubwa Kimyaaa!!!
Kwa mawazo yangu ni Mkali wa hizi kazi na uzoefu unachangia.
Nilikuwa napanda wakati ule kabla ya Corona.
Jamaa anajua kucheza na muda, hata mchelewe vipi kuondoka arusha. Muda wa kufika Shekilango haupishani kwa zaidi ya dk 5.