Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

way back 2015 au 2016 hivi mida ya saa nne kasoro usiku natoka mwenge narudi home kimara na washikaji kufika hapa mataa ya chuo kuna jamaa na hardbody akaja akaparua gari upande wa kulia na mbele tena akaparua premio... kwasababu kulikuwa na jam akasimama.... nikashuka kumfuata Ile nafika tu pale jamaa akaanza kutema mbovu pale maana alikuwa kikombe tayari, wenzio wamekaa kimya tu. taa zikaruhusu jamaa akatia gear chap ikabidi nindandie chap nyuma na kuwaambia jamaa zangu waendelee na safari Mimi nicheze huyu mkushi. basi chuma imeenda hadi mataa ya tabata Mimi nipo nyuma nikaona kwa huu uendeshaji huku nyuma si salama kwangu ikabidi pale mataa niite boda nimekuuliza una mafuta ya kutosha jamaa akadai ndio ikabidi nipande boda na kumwambia fuata hii gari.... mataa yakaruhusu jamaa akang'oa na sisi tukang'oa na boda... kufika buguruni jamaa akashika njia ya kkoo mpaka mataa ya ilala, pale akashika njia ya keko mpaka taifa, taifa akashika Mandela mpaka tazara na kukunja kushoto uelekeo airport ila pale akasimama kumshusha mshikaji mmoja hivyo kwenye gari wakabaki wawili dereva na mmama na na mimi nilishuka pale kwenye boda kumfuata ila aliendelea kuongea mbovu.. basi pale safari inaanza tena, jamaa alitupeleka mpka chanika huko mbali sana na mpaka tulipokuta kapata ajali nyingine tena ya kugonga Carina na yeye gari yake kupinduka. sasa huku nyuma kumbuka alitugonga wawili kumbe Yule mdada alikuwa ni mjomba wake na kova so taarifa ilikuwa ishapelekwa na Yule dada aliomba mawasiliano yangu kwa jamaa hivyo baada ya kuwa tumemdaka nikamjulisha Yule dada ndani ya dakika 10 ikaja pale cruiser police wakaniambia tu wewe nenda ila asubuhi saa nne uende pale urafiki kituo cha police.... asubuhi nikafika pale nikamkuta mkushi kawa mpole kuliko maelezo kama sio Yule wa Jana plus Yule dada ... ikabidi mafundi waje pale wakadirie gharama na jamaa akatoa... sijajua walimalizana vipi na wa CARINA maana ilikuwa haifai.... kama upo humu nisamehe bure ila hukuwa muungwana ndo maana tulifika Ile hatua...
 
Hizo gema ni balaa kuna mahala baada ya Gairo kuja Morogoro zipo nyingi; siku moja kidogo gema zinipeleke korongoni aisee. Hivi hawa majamaa wanapopita na ma 'viete' yao uwa hawaoni jinsi barabara zilivyo mbofu mbofu??
 
Wese kutosha ni jambo moja, kuna mwingine anapenda gauge ikisoma half tank tu ajazie tena. Gauge iwe inapepea kama bendera full time

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
That's me! Ikifika half tank tu, najazilizia. Haswa kwa kuogopa lolote kutokea na kujikuta unalazimika kuingia kwenye vituo vya mafuta ya kubumba. Hivyo ujazilizia kwenye vituo vya Total kwenye miji mikubwa.
 
Ila ya nzega kwenda tabora, ni finyu tu ila hakuna matuta . Hata ya kwenda kwa Presidaa ukiwa watokea kahama kuna sehemu unateleza na zote.
 
Hizo gema ni balaa kuna mahala baada ya Gairo kuja Morogoro zipo nyingi; siku moja kidogo gema zinipeleke korongoni aisee. Hivi hawa majamaa wanapopita na ma 'viete' yao uwa hawaoni jinsi barabara zilivyo mbofu mbofu??
Ya seriakili hawana uchungu nayo asee.. ila kama ni gari yako lazima uwe mpole, hasa kwa sie wapenzi wa sedan tunakuwaga na utii kwa barabara isiyo eleweka
 
Polisi labda uone hawana alternative ya usafiri sio wamepaki Cruiser lao we unajifanya kuwakimbia [emoji23][emoji23][emoji23] wakikuungia ni msala!
Na kuna wale polisi huwa wanaweka barrier.

Wanakupiga kaa kushoto, ukijidai kukimbia wanakupasua hutaamini.

Wale watii, hata wakikwambia piga jeki tukague kwenye uvungu wewe tii tu.
 
Unaweza ukawakimbia ukadhani yameisha.

Wanapiga simu mbele unakuta road block.

Wanakuweka kati.
 
Na kuna wale polisi huwa wanaweka barrier.

Wanakupiga kaa kushoto, ukijidai kukimbia wanakupasua hutaamini.

Wale watii, hata wakikwambia piga jeki tukague kwenye uvungu wewe tii tu.
Wale wa barrier usiku watamu sana aisee, waweza kuwa umetoka zako huko kibatiiii chombo inavumaaa wanakupiga tochi pwaa pwaa pwaa ili usimame, unapoza chombo unasimama ukiwafikia salamu tu washa taa za ndani kukagua kawaida tu kama kuna sehemu kuna kicheche wanakwambia la wanakuasa tu mdo mdo, kibatiiii Mzee. Safari usiku raha sana
 
Sasa huku kwetu barabara zikipita watu wanakuja kuanzisha makazi pembeni.

Hata uifiche porini vipi, kesho kutwa unakuta kimji hapo.
 
Unaweza ukawakimbia ukadhani yameisha.

Wanapiga simu mbele unakuta road block.

Wanakuweka kati.
Huwa inatokea. Na hapo kama wamea amua kuwa serious kabisa na wewe. Ila kama walikuwa wanataka wakupige hela wao kama wao. Msala huwa unaishia hapo, maana kwanza ahawajui unaelekea wapi . Na pia yule hata wange fanya hivyo ningekuwa ni mimi bado ningejitetea, jamaa walikuwa hawana uniform na wala reflector unaaminije kuwa wale ni askari ? Japo siungi mkono ukimbiaji wa Trafic
 
Upo vizuri sana.
 
Ile barrier kabla ya KIA huwa naisahau sana.

Kuna siku nilikuwa naovertake hamadi barrier hii hapa. Wanakupiga tochi ukae pembeni.

Uzuri wa pale wanakagua magendo tu. Mambo ya kuovertake hawana time na wewe.
 
Ukiwa highway mfano segera, gari ya safari ndefu inajulikana na gari ya kuishia kimji kinachofuata inajulikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…