Wazee wa β€˜Road Trip’ mpo?

Journey mercies [emoji1488]

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
Gracias. Uneventful journey. Japo nilikuwa man alone kwenye gari.

Asubuhi nilimpa lift askari from Mwanga to Moshi so nimetembea kibabe, full kutanua na kupita na 50. Nikipigwa mkono anapewa salute natembea. Nimependa haya maisha dah

Road is beautiful as always.
 
Asubuhi nilimpa lift askari from Mwanga to Moshi so nimetembea kibabe, full kutanua na kupita na 50. Nikipigwa mkono anapewa salute natembea. Nimependa haya maisha dah

Road is beautiful as always.


Aiseeh ilishanipata hata mie safari moja wakati naichakata lami, nikapigwa mkono na askari pale Chalinze, nikajisemea huyu anataka nini tena...!! Maana ilikuwa bado alfajiri, mambo ya kuondoka Dar saa kumi kasoro alfajiri...

Nikavuta pumzi ya kujiamini nikasimama nikashusha kioo, akakagua vibali viko sawa akacheki system yao sina fine iliyo pending...

Akaniuliza, mrembo alfajiri yote hii unaenda wapi na unatoka wapi....!!!

Umekumbia majukumu au unaenda kufumania ...!!

Nikajikuta nacheka kisha nikamjibu uelekeo wangu.
Akasema naomba lifti....

Daah ikumbukwe hapo nimefika chalinze bado hakuja pambazuka kuna kagiza giza halafu niko peke yangu kwenye gari, tinted kama zote.


Nikajiuliza, je nikikataa itakuwaje...!! Nikimkubalia je nikifika kwenye pori akinigeuka, japo alikuwa na uniform what if ni tapeli, uniform mtu anaweza zipata... daaah...!

Nikamuuliza unaishia wapi, akasema utaniacha (.......) akataja anaposhuka.

Nikasema, falailahi....

Nina nia nzuri Mungu atanilinda.

Nikaanza kufata sheria kwenye 50 natulia, pasipo ruhusu kuovertake natulia.

Akaniambia, ukipata upenyo we nyooka atayekusimamisha washa full light halafu fungua vioo wakiniona poa hakuna kusimama.

Weeeweeeeee, nilikaza taqroo hadi namshusha, yuko daah. Uko vizuri....

The End😜.
 
Safi sana.
 
Na kilometer 1700 hivi za kuchabanga katikati ya weekend ya pasaka na karume day.
Na mikoa 6 ya kukatisha
Mimi jana nilipiga 1300km in 26 hours. Niligeuza the same day jioni kutoka Arusha nikarudi Dar.

Fatigue ingeniua.

Niliona reaction time yangu imekuwa mbaya mno, ikabidi niache kumwaga moto nikawa naifuata gari nyingine nyuma namtumia kama guide wa kuniangaliza mbele.

Kufika mombo nikakunjua kiti cha abiria nikajilaza, nkashtuka lisaa limoja na nusu baadae nikiwa fresh. Ikawa ni kulala na kona za korogwe tu - sedans zina raha yake kwenye curves.

Fatigue is real. Usingizi hauna baunsa.
 
Dah upo vizuri mkuu, hakika usingizi lazima utakua ulikukomesha.
Hapo utakua ulikua unasikia nyuki muda wote.
Mimi sitaki stress na siku kama 4 za safari.
Day1: 450 KM
Day2: 380 KM
Day3: 600 KM
Day4: 450 KM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…