Wazee wa β€˜Road Trip’ mpo?

Ile michezo ya mtu katoa na wewe unatoa bila kujihakikishia ndio inakuwaga na majibu haya.
Siyo michezo mizuri kabisa. Almanusura uso kwa uso na lori maeneo ya Kongowe.

Kuna jamaa alikuwa na X3 sasa alikuwa mbele. Jamaa alikata lori moja nikawa nipo nyuma yake. Sasa ile kumaliza tu, kama mita 50 hivi au pungufu, lori hilo hapo. Bahati nzuri nikawa nami nimelimaliza lori.

Nilienda na hiyo X3 kwa umbali mfupi tu, ikabidi nimpite maana mvua zilikuwa zikinyesha na jamaa aliyumba kama mita 70 hivi. Pamoja na mimi kufanya kosa la kumfuata huyo jamaa, ila jamaa hakua dereva mzuri. Hivyo ilinilazimu nimpite tu pamoja na kutaka ligi.

Barabarani kuna vituko na mambo yanayohitaji umakini sana.
 

Duuh..... hadi roho imeniuma maana ....!

Asante kwa somo.
 
Ha ha ha hivi ushaona madereva wetu? Mmoja akitoka wote wanafuata kama nyumbu? Huwa najiuliza hawa wana akili kweli?

Aahahahahahhaaa.....

Najitahidi sana mara nyingi nnapotoka na chombo cha usafiri niwe ndani ya muda au nina muda wa ziada wa barabarani kuepuka kuendesha kwa kukiuka miiko ya udereva.

Hivi ushawahi kuwa kwenye hali ya kuwa nyuma ya muda nusu saa au saa nzima na kuna msongamano wa magari barabarani?

Japo baadhi ya madereva hawasikii raha hadi waendeshe kwa kukiuka miiko, siku likitokea la kutokea wanasema ajali kazini.....!

Stress za wese kukata pia zinachangia 🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…