Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Pale mikumi hatari sana kukatiza kwa speed zaidi ya 120

Wanyama ni wanyama tu

Unaweza kuona peupeee mara pAAAp, tembo anavuka, ama nyumbu, ama Nyati (sipati picha)
Najua mkuu...
Mara ya mwisho nimepita hapo almanusura tumvamie swala alikuwa sijui anaharakia wapi kakatiza toka upande mmoja kwenda mwingine, tulikuwa kwenye ligi na jamaa mmoja hivi...chuma ishakolea ipo kama 160kph hivi, uzuri alipita spidi sana hatua moja tu ndio aliyokanyaga lami ya pili akawa kashapotelea machakani...

Ila ndio unajua tena ukishakuwa dereva uliyozoea kuchapa lapa, kuna roho ya ujasiri unakuwa nayo...
 
Nilishawahi kupita huku 2016 au 2017 hivi.

Kila unaemuuliza anakwambia utekaji upo kama kawa.

Njiani tukakutana na askari polisi wakatuambia kuna tukio limetokea dk 10 kabla hatujafika.

Toka siku hiyo hii njia naiheshimu vibaya mno.
 
Nilishawahi kutoka morogoro saa 12 jioni nikafika dar saa 7 usiku. Kuna lari lilizima hapo gogoni.

Juzi kati nimetoka mbezi mwisho saa 12:30 asubuhi nikapita chalinze saa 3.30 asubuhi.

Mwezi uliopita nilitoka ubungo saa 5 asubuhi, nikafika vigwaza saa 11 jioni. Walikuwa wanaweka zege maeneo ya kwa matiasi.

Sahivi hata kama naenda chalinze, nazungukia bagamoyo - msata. Morogoro road ni kichefuchefu.

Morogoro road hapana kwakweli. Hii njia imekuwa kichefuchefu.
 
Hiyo labelling ya 'balaa jingine hili' inathibitisha upekee wa hii makitu [emoji4][emoji4]. Difference kuu ya Dom - Mza na Dar - Mby ni high traffic, njia ya kwenda Mby huko magari mengi sana. All in all daah kuachieve hii kitu ni mguu na kibati mwanzo mwisho aisee
 
Kwa barabara zetu kupata average speed over 100kph inabidi ukimbie sana.
 
Dar iringa 501km
 
Nissan patrol ya kwaza. Kuendesha ilikuwa ya mzee fulani wa dodoma , trip ya dar to dom , gari ilikuwa auto halafu sijui kwa nini halikuwa na nguvu kabisa na ndio lilikuwa linetoka japan. toka siku hiyo nikayachukia kabisa hayo madude ,
Ila must admit, zipo comfortable sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…