Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Tire niliangalia brand na zilivyo kwenye hali ya upya siku zichunguza sana, hata Extrovert alizikubali sana, maana nilikua nae wakati naenda ichukua, nahisi zime expire na hatukuangalia
Yeah tyre ile ni Bridgestone Nextry sema kwa namna ambavyo ilikuwa imeshiba sikufikiri zingekuwa na tatizo! Tia Pirelli kama ukikosa Micheline Premacy
 
Mzee unapiga roadtrip si mchezo! You are my role model!

Mimi nimewahi kupiga roadtrip za siku kadhaa mfululizo mara mbili tu na zote ni za kikazi tu! Ya kwanza ilikuwa Dar-Tanga-Kilimanjaro-Arusha. Ilikuwa ni safari ya usiku na mchana hakuna kupumzika na haikuwa safari ya moja kwa moja bali tulipitia kwenye wilaya kadhaa safari ilianzia Dar jioni via Bagamoyo, tukaingia Msata then tukaingia Tanga.

Tanga tulipitia wilaya za Korogwe, Handeni, Muheza, Pangani na Tanga mjini. Kilimanjaro tuliingia Mwanga ndani ndani, Moshi ndani ndani, Hai ndani ndani, na Siha ndani ndani then tukaenda Arusha mjini ambapo ndiyo ilikuwa mwisho wa safari yetu na pale ndiyo tukatafuta hotel tukapumzika.

Maana safari nzima tulikuwa tunalala kwenye gari then tunaamsha, na kulala kwenyewe ni nusu saa hadi lisaa limoja imeisha hiyo, maana tulikuwa watatu including dereva na dereva akawa anatuambia tusilale tumpigishe story ili asije akasinzia akachochora. Yaani tulikuwa tunashuka sehemu kula tu au kuchimba dawa na kuoga kwenye hivi vyoo na mabafu ya kulipia basi so tulivyofika Chuga ndiyo tukapumzika.

Tukajipa siku nzima off ambayo ndiyo tulipanga tulale hiyo siku nzima halafu kesho yake ndiyo tuamshe kurudi Dar. Wenzangu walikuwa wamechoka wakalala kama pono ila cha ajabu mimi kulivyokucha ndiyo kwanza nikawaacha, nikaingia town pale nikazurura kidogo then Baadaye nikaenda Rombo nako nikazurura kidogo hadi jioni then ndiyo nikarudi Arusha, kesho yake sasa ndiyo tukaamsha kurudi Dar.

Ya pili ni hizi za juzi hapa ila hizi angalau zilikuwa siku chache na hazikuwa za usiku na mchana maana tulifikia Mbeya mjini. Jumamosi ilikuwa Dodoma-Mbeya, Jumapili ilikuwa Mbeya-Chunya (kwenda na kurudi), Jumatatu ilikuwa Mbeya-Kyela (kwenda na kurudi) na jana Jumanne ndiyo tukaamsha Mbeya-Dar.

Mimi ninavyopenda safari yaani hata nisafiri vipi huwa niko fresh tu tena kadiri ninavyozidi kusafiri ndivyo ninavyotamani nisafiri zaidi na zaidi nifike sehemu ambazo sijawahi kufika. Yaani nimejigundia napenda sana safari na safari inapoanza huwa sitamani tufike tunakoenda sema tu ndiyo hivyo kazi haziruhusu.

Nawaonea sana wivu watu wanaofanya kazi zinazowalazimu kusafirisafiri kila mara na mimi starehe yangu siyo kuendesha bali kuwa mbele pale pembeni ya dereva mimi ndiyo huwa naenjoy zaidi. Mfano zile safari ambazo mnatakiwa mpeleke mizigo kwenye mikoa mbalimbali halafu mko na cruiser ama coaster wawili au watatu tu dereva na utingo halafu safari iwe day and night yaani huwa nafurahia acha kabisa.

Naamini huu kwangu ni mwanzo tu natamani ifike kipindi nipate safari za mfululizo kama wewe hadi nizikimbie mwenyewe. Halafu mimi sichaguagi usafiri mimi gari, meli, ndege au treni vyote twende tu tena huwa naenjoy slow transports kuliko fast ones mfano meli na treni, unless iwe ni safari ya dharura na haraka ila tofauti na hapo sipendagi haraka kwenye safari zangu, yaani mimi nikiambiwa meli au treni tunayopanda itachukua kuanzia siku mbili na kuendelea kufika tunapoenda ndiyo huwa nafurahia kweli yaani, mradi tu kuwe na basic needs pamoja na some luxuries humo ndani.
Hahahah unatufaa wewe 😅😅😅
 
Hii gari niliipa sana sheeda ya kutosha. Nilinunua 2013 ishapiga sana arusha mwanza singinda huko nzega sijui wapi. enzi hizo ninayo mm na mwarabu mmoja hivi yupo Upanga. After few years nikaona vijana wananunnua nnua kama njungu. sasa mm nikaiuza. Sasa hivi nimehama huko nipo kwenye V8 ya Chini, Majesta gear 8. chombo ninatizo kina hama kama akina akili nzuriView attachment 1811789

View attachment 1811792
Nikajua umehamia kwenye IST ungezingua sana! Ila kwa MAJESTA ni Nuff Respect! Umeme huo naukubali sana comfortability na mwendo at the same time
 
Kuna gari zina sensor kabisa.

Tyre pressure ikiwa ndogo inakulimit kwenye speed na kukupigia alarm. Au kama unatumia tyres ambazo hazipo recomended nako zinakupigia alarm kwamba usizidi hiyo speed.
Mimi natumia common sense tu. Hakuna kitu kizuri kama kujua limits zako. Kila gari ninanyoendesha najitahidi nijue limits zake na si kufuata kisahani au ligi na mtu.
 
Back
Top Bottom