Kweli mkuu sijui umetumia gari gani ila mfano kama LC V8 zina uwezo wa kutumia 4hrs tu from Dar to Dom ndiyo maana hata viongozi wakubwa wanaoendeshwa kwa hizi gari wana uwezo wa kuja Dar kila ijumaa jioni kuspend weekend nzima na kurudi Dom kila jumatatu asubuhi kuendelea na kazi! Wenyewe wanakuambia Dom hakujachangamka hivyo hapafai kula bata ndiyo maana wanatamani kurudi Dar!
Kuna siku Mwendazake alikuwa Mbeya na msafara wake imagine from Tukuyu to Mbeya mjini kwa gari za kawaida ni mwendo wa karibu lisaa na nusu lakini LC V8 za msafara wa Rais zilitumia nusu saa tu from Tukuyu to Mbeya! Yaani Mbeya mjini gari zote ambazo zilikuwa kwenye barabara ambayo msafara wa Rais ulitakiwa upite zilisimamishwa Mwendazake akiwa Tukuyu na baada ya nusu saa msafara ukawa umeshateremka Mbeya mjini!
Kwa sie SUV enthusiasts tunaona hapa kweli mjapan alitulia! Ndiyo maana binafsi kwa SUVs za mjep nazielewaga sana LC VXR V8 na NP Y62 V8 hizi gari huwa naziheshimu sana ni moto wa kuotea mbali!