Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Hamumpati mtu [emoji28][emoji28][emoji28] wewe nahisi mjeda kitengo
Lakini hivi ni kwanini watu wengi wakijua mtu ni mwanajeshi ni kama wanaanza kumchukia fulani hivi hasa hapa bongo?

Hili nimeliona kwa baadhi ya watu ambao unakuta kabla hawajanifahamu tulikuwa marafiki wakubwa tu tunaongea tunacheka na hakukuwa na shida yoyote ila baada tu ya kujua kuwa nami mmoja wao wakaanza kama kupunguza urafiki!

Sasa mtu unabaki unajiuliza shida nini maana kama wanasema eti wanajeshi ni wababe na wakorofi mbona kipindi chote cha urafiki wetu tumeishi vizuri tu na wananijua fika kabisa kuwa siyo mkorofi sina chuki na watu ni mtu poa tu kwa kila mtu!

Sasa huwa mnachukia nini mnashindwa kueleweka shida ni tabia ya mtu au ni kitendo tu cha yeye kuvaa yale magwanda?
 
Sema wanajeshi hawana shida. shida iko kwa watoto wa siro
 
Kwani nyinyi huwa mnajionaje? Kuvunja sheria barabarani mnaona ni sawa? Watu wamekaa foleni mnakatiza mbele, magari yanapita taa ya kijani nyinyi mnapita nyekundu? Mnakwangua magari ya watu mnaondoka kisa mnaamini hawawezi kuwafanya chochote? Mnapita wrong side of the road na kusababisha watu waingie mitaroni?! Watu asubuhi wanawahi kazini nyinyi mnakimbia mchakamchaka katikati ya barabara na kulazimisha magari yawafuate mwendo wenu! Watu kama hao unawapenda vipi?
 
"Watu wengi" wanamtazamo hasi kuhusu wanajeshi, na hii inatokana na sumu waliolishwa kwenye story za chini mti, kua wanajeshi wako vile...wako hivi sasa mtu anazidi kukua na mtazamo huo huo hasi. Wengi wanafanyaga "fallacy of generalization", kosa/ udhaifu wa mwanajeshi mmoja unachukuliwa kama ndo wanajeshi walivyo.

Mimi personally Wanajeshi nawakubaligi sana, masela zangu wengi niliokua nacheza nao kitaa enzi hizo tukiwa watoto sasa hivi wote ni wajeda, ni mimi tu ndo nipo 'odd one out', muda mwingine naumiaga kwa hilo😂.
Wananiokoaga sana nikiwa chuga, hawa vijana wa Simon Sirro wakiniletea pigo za kiree barabarani, sijui tyre limekosewa angle of rotation sijui wiper imekuaje...napiga tu simu moja chaap either Monduli au Tengeru, vijana Siro wananitema nami nasepa mdola mdola huku roho yangu imesuuuzika😁.
Wanajaeshi ni watu poa sana
 
Wengi wanaoogopa ni watu wenye impact kwenye serikali,wanaofanya vitendo viovu nk...
The rest ni wafuata mkumbo tu na ndio wengi.

Kuna watu huwa wanafwata tu mkumbo kuogopa,ila ukiuliza hata anaogopa nini hajui!
Eti kukamatwa!! Jamani unakuta mtu hana impact yoyote kwa serikali... Halafu anajiogopesha.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…