Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Sanamu langu mnajenga lini?

Nataka likae pale pembeni ya kibanda cha hamza nje ya ubalozi wa ufaransa.
 
Nisharudi. Nimeingia jana usiku. Nilikuwa nakimbizana na Discovery 3, vichwa nilivyopakia waliomba mpaka namba next time wakiwa na safari wanicheki kwanza niwabebe tena, wanasema it was an experience [emoji38][emoji38]

Niko mjini, nipange
Umerudi[emoji847]

Wameomba uwabebe tena mzee wa mambio[emoji38].
Wewe kwa mbio zako ungenifaa sana kwa safari zangu za asubuhi...yaani huwa nafurahi sana dereva akikimbia,,tuwahi kufika.


Nimekumiss sana aisee,i want to see you [emoji6].
Twende zetu Kimara kwenye mkutano wa Imani, upendo na miujiza.
 
Vyombo vipo? Ikiwa naruhusiwa kupokea neno huku nikiwa na red cup yangu mkononi ina mchangayiko wa kvant na stoney tangawizi kwa kufuata ratio za mkemia mkuu ntaweza kuhudhuria mkutano. Ila kama waliookoka watakuwa wananijaji na kunitolea macho ya chuki hapo hapatanifaa.

Jana nilifikia kiwanja kwanza kutoa uchovu wa safari. Zilipigwa gospel live band almost 30 minutes pale tukapata upako wa kutosha na nguvu ya kuagiza round nyingine. Mungu ni mwema.

Nilitamani sana nikurekodie video
 
[emoji38]twende tu na kvant zako,,,hakuna tatizo kabisa.
Haya jiandae,saa9 nakuja kukuchukua[emoji6]
 
Kuna msemo unasema jeshi ndiyo lenye nchi yaani wanajeshi ndiyo wenye nchi. Huu ni msemo wa kizushi tu ila hao wanaofanya hivyo ni vikosi maalum ambavyo majukumu yao huwaruhusu kufanya hivyo tena wakiwa kwenye magari ya jeshi au wakiwa wamevalia combat tu na siyo wakiwa kwenye magari yao binafsi au wakiwa wamevalia kiraia hawaruhusiwi.

Na ndiyo kama nilivyosema kuwa siyo wanajeshi wote wenye ubabe na usumbufu kama huo kuna wengine wako cool tu hawanaga muda wa kusumbua raia. Na tukumbuke kila kada nchi hii zina watu wanaojitambua na wasiojitambua hivyo kuijudge kada nzima kwa sababu ya baadhi ya watu wa aina hiyo siyo sahihi hivyo siyo wanajeshi wote ni wakorofi.

Halafu mbona hata viongozi wetu huwa wanasababisha msimamishwe na mchelewe kazini kwa sababu ya misafara yao isiyoisha lakini hamuwachukii eti jamani [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Yeah wanalishana sumu huko na kutuchukia tu bure bila sababu halafu wakitaitiwa huko wanatupigia simu kutuomba tuwasawazishie msala. Mwanajeshi ubaya wake utauona pale ambapo utaingia kwenye kambi ya jeshi halafu unaulizwa maswali husomeki majibu yako kisha yakakukuta ya kukukuta.

Na vijana wengi story zao ndiyo hizo utasikia eti kuna jamaa sijui alikatiza kwenye kambi ya jeshi akapewa adhabu ajaze maji kwenye pipa kwa kutumia kisoda. Yaani vijana wakikaaga kwenye vijiwe vya kahawa huwa wanajazana ujinga mwingi sana ambao kwa asilimia kubwa hauna ukweli wowote.

Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo raia wake wanalichukia jeshi lao bila sababu za msingi wakati hao hao ndiyo wanawategemea walinde mipaka ya nchi yao [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wala siwachukii huwa nawashangaa tu at the same time mtu akisema anawachukia simshangai.
 
Yeah wengi wanaogopa kwa kufuata mkumbo na kulishwa sumu tu. Na hata kama mtu angekuwa anafanya maovu siyo kazi ya mwanajeshi kumkamata na kumuadhibu huyo mtu hiyo ni kazi ya polisi.

Wanajeshi hatukamati wahalifu walio ndani ya mipaka ya nchi. Maadui wa kwanza wa wanajeshi ni waasi au magaidi kutoka nje ya nchi ambao wamevamia mipaka ya nchi yetu hao ndiyo tunadeal nao.
 
Duh kwahio wewe unasema zile adhabu za ajabu huwa hamna? Na wewe Una generalize sio waTz wote wanachukia wanajeshi au polisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…