Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Kuna siku tunatoka Morogoro tupo kwenye Nissan Patrol Y60, Kutoka Kingolwira kulikuwa na Traffic baada ya kipande hicho kuitafuta Mkambarani. Abood ikawa inataka iochomoe ikae mbele, baada ya kuona mwenzake New force kaovateki gari 2 kisha akaomba kuingia.

Mbele wakati New Force anaingia alipiga honi Kwa fujo mpaka dereva wa Harrier akaingia pembeni nusu ahame njia. Sasa Sisi nyuma yetu Abood alikuwa anatoa gari mpaka usawa wa mlango wa nyuma Kwa abiria na anapiga honi Sana na kuwasha taa Kwa fujo na konda anatoa mkono kutupa ishara ya kupunguza mwendo. Sisi tunatembea bila wasiwasi jamaa walikuwa kila akitaka atoe anakuta wala hatuami.

Nyuma ikatokea Kidinilo ilikuwa imeovateki mpaka Abood sasa inataka ikae mbele yetu na imekaribia mpaka usawa wa mlango wa dereva kisha anapiga honi Kwa fujo na lesi hatua chache mbele roli likatokea saiti ambayo basi lipo, Kidinilo kwenda mbele hawezi sababu ya urefu na mwenzake Abood anamkazia kuingia. Ikabidi roli lipunguze mwendo Kidinilo ikakaa nyuma yetu.

Hizi basi dawa yao ukiwa na Land Cruiser au Nissan Patrol unaweka bull bar na side bar tuone kama yupo tayari kuchubua rangi ya basi kisa anataka aovateki kuwahi kukaa mbele.
 
Yaan wana tabia mbayaaa. Wameshauza uhai wao aisee. Hawaogopi hataaa. Wana laana kweli kweli
Hao wa mabasi ya kichina wachumba tu, ukiwa na Nissan Patrol au Land Cruiser unaiwekea Bull bar na Side bar pembeni kuanzia juu na chini.
Hizo basi za fiber glass akifanya mbishi anaharibu shoo na body ndani ya Dakika chache amtie hasara bosi wake Kwa uzembe.


Hiyo Side bar protection unaizungusha mpaka juu na sehemu ya nyuma.
 
Kuna mmoja tulimuweka ndani.. alikuwa anafanya ujinga. Kumbe ndani nimebeba wazee wa kazi. Tulimsubiri katembeea wee tulipokaribia na kituo cha polisi, tukavuta tukapiga block. Akashushwa .. ndani siku moja 😀😀😀😀 wajinga sana wanaweza kuua hawa ukiwachekea chekea
 
Ha ha ha ha mna roho ngumu sana aisee. Yaani bodi ya gari na tako[emoji23][emoji23]
 
Hahahaha hivi hizi ngap si walishakataza mkuu? Maana enzi hizo magari wanaweka ngao mtu anakuletea yote na huna pa kutokea. Ofcourse wako mnaiwakazia kama.nyie. mimi hata siwezi
 
Ila barabarani pia hata huku mjini nimekuja jifunza usiige watu. Mfano ukaona mtu anatembea mwendo hata kama ni gari yabkawaida usiige. Huko kwenye mwendokasi ukiona mtu anapita usiige. Huko road watu wanavyokimbia usiige. Huwa maafisa vipenyo wanakua na mishen zao wanawahi[emoji23] we unasema uunge upige nae battle. Mnashikwa we kila mahali unakila cheti we unaishia kula vyeti tu mwenzako anasimama wanasalimiana safari inaendelea. Uwe na hela za kiwi za kutosha
 
😂😂😂 barabarani sio pa kuigina.. kuna kila aina ya watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…