Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Gambling Table angetumia Dar Express kama anatokea Rombo kwenda Dsm au Ester
naona Kilimanjaro Bus km linaanzia Arusha Moshi - Dsm na kurudi Arusha, km ni yale ya yule Mama
ngoja wazoefu wa Rombo wakuje
Nakumbuka kilimanjaro walitangaza safari ile Oct kuanza tena kwenda route ya Rombo. Sina hakika kama walienda ama lah. Hii route ya Rombo huwa ni ngumu sana kwa ambao si mabasi ya wazawa. Dar express anakazaga tu lkn ni ngumu na ni hivyo wana abiria wao wa permanent. Ila hii njia ni ya Esther na Tilisho. Nikushauri upande Tilisho ndo naona wastaarabu sana
 
Pole sana...mimi huyu dereva wa basi aliamua tu kunikomoa...ninakaribia kumpita ili nilipite lifuso la mbele, jamaa naye akahama lane ili alipiye lile fuso....sikuwa na namna zaidi ya kutafuta lane nyingime ambayo ni majani huko nje ya barabara..
Nakuelewa sasa kaka.Formula yangu barabarani-any driver akinipigia makelele ya horn si respond as long nipo sahihi au nimeshafanya maamuzi ninayoona ni sahihi.Ajali nyingi sana hutokea mtu anapokuwa distracted in a less than 30 seconds.Huyo dereva wa basi hopeful in less than 30seconds angeweza kukuua kwa udereva wake wa kipumbavu.
 
Kuna kipindi zilikatazwa kwenye magari ya abiria mabasi na madaladala....sasa sijui kama wanaruhusiwa
Offshore Seamen Ngao zilikatazwa nakumbuka Malori na Mabasi wakati huo Scania waliweka Ngao za kutisha za kuchonga, na ilitokana na matukio waliyokuwa wakiyafanya pale Kibaha na kupiga zile horn mfano wa tarumbeta.
siku hizi gari km L/cruiser na Prado naona zinakuwa special zinakuwepo
 
Kuna kipindi zilikatazwa kwenye magari ya abiria mabasi na madaladala....sasa sijui kama wanaruhusiwa.
Nilikuwa naongelea private car. Kwenye mabasi naona Asian Star zinakuja na ngao kubwa, Ila Golden Dragon zinakuja na ngao ndogo.

Mabasi wasiwaruhusu ngao maana wao wanatabia ya kutokeza mbele wakiamini wataachiwa wapite hata kwenye eneo gumu, matokeo yake watakwangua gari ndogo.
 
Kabisaa mkuu...bahati nzuri ilikuwa ni sehemu nzuri ya tambarare....ingekuwa ni milimani...Historia ya marehemu ingesomwa....Marehemu alizaliwa, akakua, ananunua gari, akafa..[emoji119][emoji38]
 
Kwa magari private sina info zaidi...ila naona baadhi ya Land cruiser, Nissan Patrol na Suzuki escudo baadhi watu wameweka za kuchonga...sijajua wanaruhusiwa au wanafanya kibishi..
 
Nilikuwa nazungumzia upande wa gari binafsi ambazo ni SUV.
Kwenye mabasi zile ngao zilikuwa ni hatari ingawa saizi Asian Star zinakuja na ngao moja Kwa moja hata Golden Dragon.
 
Yes. Walikataza. Sijawahi sikia wameruhusu tena mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…