Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Mazee ndizo baraka zenyewe hizo. Hizi material things saa zingine uwa tunazithamini kupita kiasi. Hivyo nyakati zingine ukiamua kutoa sadaka, hakika hata Mungu anazidi kukubariki.
 
Dooh natamani siku hata ikitokea bahati mbaya nimegonga gari ya mtu basi awe mwenye mioyo kama yenu

Huwa tunashuhudia watu wanavyokula makofi mbele za watu kama watoto wadogo si mchezo

Na hata mimi mtu akigonga gari yangu huwa sijuagi kuwaka kuanza kumtukana au kumpiga

Sema majibu yake ndiyo yatadetermine nimchukulie hatua gani maana kuna wale wa "kwenda huko utanifanya nini"

Kuna mtu aliwahi kuvunjiwa ufunguo wa gari lake hivi hivi kisa majibu yake ya shombo na wakati kosa ni lake
 
Mazee ndizo baraka zenyewe hizo. Hizi material things saa zingine uwa tunazithamini kupita kiasi. Hivyo nyakati zingine ukiamua kutoa sadaka, hakika hata Mungu anazidi kukubariki.
Ni kweli mkuu, maana kuna leo na kesho ..unaweza ukamkazia mtu kamkwaruzo kwa elfu 50, kesho ukajikuta umegonga Range Rover la mtu la mwaka 2019..
 
Na mara nyingi ukiona mtu ameguswa kidogo huko bara barani akaanza kumshambulia mwenzake kwa makofi au matusi mazito, basi huyo ni limbukeni wa gari au ni limbukeni wa matumizi ya barabara.......
Mtu akishatambua kwamba barabarani kuna kukwaruzwa au kukwaruza gari la mtu, kazina awe muelewa...
 
Haha usikute ndiyo wale aliokuwa anawasemea 9.8ms squared kwamba akipindua IST tu anachanganyikiwa. Sasa mtu kama huyo umkute kajichanga kavuta zake BMW halafu ujichanganye ukamgonge weee huwa wanasahau kabisa kwamba haya mambo ni ya kibinadamu tu na kuna leo na kesho. [emoji3][emoji3]
 
Siwasemi vibaya ila madereva wa IST wamechangamka sana kama wa subaru watata sana..
 
Kwenda huko

Utanifanya nini[emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…