Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Ng'ombe bana, nikisafiri unakuta gari imekolea halafu wapo pembeni wanakula majani huwa najiuliza hawa ng;ombe wakiamua kuvuka hapa patatosha kweli?!!
Hahaaa ila unaambiwa bora ng'ombe mkuu nasikia ukigonga punda lazima gari iharibike vibaya. Hadi leo najiulizaga wana nini punda sijawahi shuhudia gari ikigonga punda inakuwaje.
 
Im sorry to say this lakini Bongo tunaishi tu ili mradi ndio maana ajali za hovyo hovyo ni nyingi.
Mwaka 2018 nikiwa natoka bagamoyo kuja dar nilishuhudiaga tukio la kushangaza na kustaajabisha sana, tukio lilikua hivi...

Ilikua usiku mida ya saa 4 hivi, Niko barabarani na mbele yangu kulikua na Noah ikiwa imewasha full, Sasa mbele yetu gari zikawa zikimkumbusha (zikimpigia full na beam ili kumzindua Kama kajisahau) lakini yule Noah aliganda vilevile na full yake.

Nikahisi pengine huyu ni mgeni barabarani hajui lugha za ishara, au ni dharau tu akijijali yeye... Basi mbele ikawa inakuja ile Scania tipper ya mchanga, ikampiga full na beam Kama Mara tatu hivi Noah akawa Bado kaganda vilevile na full yake, yule Scania akazima taa kabisa alafu akawasha, Bado Noah kaganda na full vile vile.

Basi bila kutarajia ile Scania ilihama mguu mmoja kutoka kwake kuja kwetu ( kumbuka mm Niko nyuma ya Noah hapo [emoji28]) nilipigwa na butwaa nikapanic then nikakanyaga brakes za ghafra Sana Hadi waliolala ndani wakaamka, basi sekunde chache tu nikashuhudia Noah ikipalazwa ubavuni maana jamaa wa Noah aliyumba kidogo ndo ikawa salama yake kupalazwa Hadi kilo Cha ubavuni upande wa nyuma kikavunjika na Scania hakusimama

Tukio hili lilinifikirisha Sana, na tangu siku hiyo huwa Niko making Sana taa zangu hasa zikitokea hizi tipper za mchanga huwa nakua making ni Sana aisee, maana jamaa wa Scania alitafsiri kaletewa dharau, akaona ngoja amuoneshe kuwa hapendagi ujinga.

Tuweni makini na taa zetu jamani Kuna watu wamepinda huko road hasa hao waendesha tipper za mchanga, si ajabu kumkuta Anapuliza bangi huku akishushia na K vant on the wheel.
 
Sure mkuu watu hawajali kabisa maana mtu anaweza kuwa anaendesha vizuri kwa kufuata sheria ila akaponzwa na wenzie wazembe wanaojifanya wajanja. Hawa ndiyo wanafanya mtu ulazimike kuendesha magari matatu kwa wakati mmoja.
Siku hizi mkuu mtu anaendesha gari tatu, boda boda mbili kushoto na boda boda nyingine mbili kulia.....Kuna wakati inafika ujuta kuishi Hapa Tanganyika..
 
Duuh pole mkuu mimi wakati najifunza niliwahi kugonga hadi ng'ombe wa watu kwenye kona ila cha kushukuru hakufa. Alianguka tu number plate ikamkata kidogo kwenye mguu.
Mtu akipata ajali huwa namsikitikia sana...
Lakini kuna ajali zinachekesha ., Nikisikia mtu kagonga ng'ombe, punda au mkokoteni huwa najisikia kucheka sana..[emoji119][emoji119][emoji1787][emoji1787]

Na punda ukimgonga na kigari kidogo, anajipukuta vumbi anaendelea kula majani, wewe unaenda garage..[emoji1787][emoji1787]
 
Nyama Yao ngumu Sana. Kuna watumishi wa govnnt waligomga punda njia ya Dom -iringa Miaka ya nyuma kidogo, hakutoka mtu.
Niliwahi pewa hii story.

Zamani miaka kabla ya Yesu, watu ambao hawakuwa na silaha kama mapanga au mikuki walikuwa wanachukua mifupa ya punda, wanaichonga fresh wanaitumia kama silaha.

Mifupa na misuli ya punda ni migumu sana kwasababu kila siku anafanyishwa kazi. Hivi vigari vidogo havina mabati ya kuitawanya ile mifupa.

Ukigonga punda ni kama umegonga ukuta.
 
Pangekuwa na ukungu kama huu ambapo unaona mita 20 tu mbele je? Angeweza kutembelea full? Full kwenye ukungu inapunguza visibility.

Hii juzi hapo makambako

 
Binadamu tuko very creative, toka enzi na hata sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…