Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Changamoto ya tatu wezi, nimeibiwa kile cha kupangusia maji ya mvua sijui waiper, nadhani nimeibiwa kwenye foleni. Natakiwa nipige libit sijui kuzunguka gari yote ili wasichomoe vitu vingine.
Ni hayo tuu madereva wenzangu
Pole sana wengine magari yetu hata tukiliacha wiki nje hamna kinachoibwa!
 
Hizo honi wala usizipuuze...
Unatakiwa kujenga mazoea ya kusikiliza sauti kutoka kila upande wa gari lako na kuzifanyia uchambuzi ndani ya ubongo wako within a second..[emoji28]..wakati huo huo unaendesha.....[emoji28]

Hizo honi kuna siku utapigiwa honi yenye maana, ya kukuepusha na majanga, ukaipuuza....hapo ndipo patamu..[emoji28][emoji28]

Endelea pia kujenga mazoea ya kuendesha gari lako, GARI lililoko mbele yako na nyuma yako, boda boda au bajaji zilizopo kushoto kwako na kulia kwako..

Mwee[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mkuu honi za madereva wa Dar ukizifuatilia utakuwa kichaa!
 
Siku akikutana na honi za madereva wa mabasi ya mikoani anaingia mtaroni mazima. Hasa asubuhi.
 
Boda bwana ukiwaogopa inakuwaga kama ndo unawaita. Hawanaga cha kushoto wala kulia kote wanaovertake tena kwa mkwala kabisa sijui wanataka usimame wapite?

Hawa jamaa siku sio nyingi watapita juu wataona ubavuni hapatoshi wana haraka sana.

Honi bwana sijui shida huwa iko wapi Dar. Aisee hizi driving schools ni za kuchunguzwa na serikali 🤣🤣 tena tume maalum kabisa iundwe

Usiwe mwepesi kuogopa utazoea tu. Kuna Malori ya mawe yale mafuso utazoea wewe keep calm hata iweje na uwe alert. Wengi mabarabarani ni wehu tu sasa lazima uwe makini times two.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…