Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Sorry naomba kuuliza hivi sheria ya kuendesha Gari hapa nchini n kuanzia umri gan? Maana mie nilkua najua ni above 18yrs, sasa week 3 zilizopita nilisimamishwa na traffic afu n mmama,

Sasa akaniuliza umri wangu nkamtajia akagoma akasema nadanganya, baadae akaomba vyeti vyangu, cha uraia, cha kupigia kura, leseni, sasa hivyo vyote kwa muda huo sikua navyo, mara akaanza kunifokea, kwanza namdanganya afu sina leseni, akanambia faini n 30k, baadae akasema na nyongeza ya kumdanganya n 5k jumla 35k, nkaanza kujitetea akasema atanipeleka police, sasa niliogopa kupelekwa police, ikabidi nitoe faini, nkatoa 40k akasema chenji hana nkamuachia, akanambia nisiendeshe tena gari hata km nna leseni, na akiniona tena atanipeleka police hatataka faini, na ile road ndo napitaga sana, afu gari nmeanza kuendesha 2020, na traffic nshawahi kukutan nao km watatu hawakuwahi kuwa tatizo.

Nipo hata sielew, kna mtu nlimuuliza alinambia pia ruksa kuanzia 18yrs, na leseni, yule mama alinionea tyuu sasa simuamini, jaman yule mama alivonifokea ile siku had nlikua naogopa mie, hebu mnijuze kwani. Naamini humu ndani ntapata maelezo ya kueleweka.
 
Kama una miaka 18 unakaza tu. Chini ya hapo uwe mpole.

Usikubali kuwa mnyonge, utawekewa bangi siku ingine.
 
Kuna feeling flani amazing, askari anakusimamisha anakuambia ume over speed, wala humbishii, ila anapokagua picha kwenye makabrasha yake anagundua sio wewe anakuambia nenda.

Hapa unauona live uwepo wa Mungu maishani mwako

Mnaotumia njia ya Moro, pale Chalinze mizani fuateni 50, jamaa wapo asubuhi wanatwanga photo.
 
Yaani askari akuambie nenda ndio ufananishe na kuuona uwepo wa Mungu maishani?
 
Hiyo 30k ulipewa receipt?

Kuendesha gari ni kuanzia miaka 18 pia traffic hatakiwi kukagua zaidi ya leseni. Sijui uraia sijui kupiga kura anakuzingua alikuona muoga.....

Muhimu kutembea na leseni au hata picha ya leseni yako.

Usipokua na leseni utatakiwa kuonyesha ndani ya siku 7. Hakuna faini ya kutokutwa na leseni.

Ulipigwa...
 
Receipt hakunipa, afu yeye alisema nipo below 18yrs ila namdanganya, kwa kweli niliogopa vile alivoanza kunifokea aaah wee kupelekwa police mie hapana, nkatoa hyo 40 chenji akawa bhana nkamuachia tyuuh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…