Sawa mkuu but unajua kwanini hawatumii kwenye gari za Europe?
Namba ya kwanza before W ina represent degrees Celcius ambazo oil inaweza ika flow na namba ya mwisho ni thickness ya oil katika operating temperatures.
Tukiangalia kwa nchi za ulaya wengi wanapata degrees below 10’C katika vipindi vya baridi. Ila kwa Tanzania huwa hatufikagi huko throughout the year. Average ni kati ya 20-30’C.
Kwa oils za gari za ulaya ndio maana wanashauri muweke 5W means oil itembee kwenye engine kuanzia kiwango cha nyuzijoto 5’C during coldstart. Ile namba ya mwisho kuanzia 15,20,30,40 mpaka 100 ndio viscosity rating kwa maana wembamba wa oil at operating temperature yani ikipata joto maana oil ikipoa huwa inakua thickened.
Kwahivyo uko sahihi kwa oil ya w40 itakuwa nzito but w50 ni nzito zaidi which i recommend kwa gari yake hasa kama yupo bongo.
Kwa gari zetu hapa bongo nafikiri kutumia 20W50 pia sio mbaya kwa sababu hali ya hewa ya joto letu mjini huwa ni 20-30’C on average so hamna ambaye gari yake itagoma kupandisha oil ila kwa mtu aliepo Arusha, Iringa au Mbeya na maeneo ya jirani huko basi 5W-30 huenda ikawa chaguo zuri zaidi maana wale wanapataga below 20’C during cold times of the year.