Wanatumia outboard engine sababu ya unafuu wa gharama ya kununua,matengenezo na uwepesi wa kuifunga kwenye boti.
Inboard engine inabidi wafunge diesel engine gharama ya kununua ipo juu, itatakiwa awe na marine gearbox na propulsion (propeller na seal zitakazo funga mwisho kuzuia maji yasiingie katika boat). Bado Hii inboard engine inahitaji utaalamu kwenye kuifunga Ili kupunguza vibration kubwa na Kuna gharama za kununua mounting za engine na gearbox.
Pia maintainance ya diesel engine ipo juu, ndio maana wanaona Bora wanunue outboard engine ambayo akiwa na Kazi anaifunga Nyuma pale na kujifungua pia services ni nafuu sana.
Kwa upande wa Huku Baharini baadhi ya majahazi wamefunga inboard engine za Volvo S80, Caterpillar na Injini za Kubota Kuna waliopata zikiwa full na gearbox na wengine wamefanya modification huku access ya hizi injini ni kubwa sababu majahazi mengi Yanausajili au umiliki wa Kutoka visiwani Kule used za Arabuni kibao tofauti na mkoani.
Pia wapo ambao wanatumia nguvu ya upepo(matanga) kwenye Jahazi Hawa Kuna ambao wanakuwa na backup ya outboard engine Kwa ajili ya manouvre wakiwa wanaingia bandari au kupaki. Au upepo ukiwa hafifu wanatumia outboard engine waliyonayo ila wengine hawana hata outboard engine wao ni upepo tu.