Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Kuna hili lingine naomba faida kidogo ...kwa maboti yanayotumika ziwa Tanganyika ni kwamba boti inakuwa kubwa sana na inabeba uzito mkubwa na inatumia outboard machine Ila Ila yenye horsepower kubwa na ikiwezekana wanafunga mbili na zinatumika kwa pamoja ila kwa ukubwa huo huo Ila yanayotumika bahari ya Hindi yanakuwa yanatumia engine za ndani.Nini haswa inakuwa sababu
 
Wanatumia outboard engine sababu ya unafuu wa gharama ya kununua,matengenezo na uwepesi wa kuifunga kwenye boti.

Inboard engine inabidi wafunge diesel engine gharama ya kununua ipo juu, itatakiwa awe na marine gearbox na propulsion (propeller na seal zitakazo funga mwisho kuzuia maji yasiingie katika boat). Bado Hii inboard engine inahitaji utaalamu kwenye kuifunga Ili kupunguza vibration kubwa na Kuna gharama za kununua mounting za engine na gearbox.

Pia maintainance ya diesel engine ipo juu, ndio maana wanaona Bora wanunue outboard engine ambayo akiwa na Kazi anaifunga Nyuma pale na kujifungua pia services ni nafuu sana.

Kwa upande wa Huku Baharini baadhi ya majahazi wamefunga inboard engine za Volvo S80, Caterpillar na Injini za Kubota Kuna waliopata zikiwa full na gearbox na wengine wamefanya modification huku access ya hizi injini ni kubwa sababu majahazi mengi Yanausajili au umiliki wa Kutoka visiwani Kule used za Arabuni kibao tofauti na mkoani.

Pia wapo ambao wanatumia nguvu ya upepo(matanga) kwenye Jahazi Hawa Kuna ambao wanakuwa na backup ya outboard engine Kwa ajili ya manouvre wakiwa wanaingia bandari au kupaki. Au upepo ukiwa hafifu wanatumia outboard engine waliyonayo ila wengine hawana hata outboard engine wao ni upepo tu.
 
Pia niliwahi kusikia nadharia kuwa wanafunga outboard engine hawa watu WA ziwani eti kwa kuwa maji Yao ni mepesi tofauti na maji ya bahari kwa kuwa mazito ......ina ukweli wowote WA hiki tunachoaminishana watu WA ziwani?
 
Pia niliwahi kusikia nadharia kuwa wanafunga outboard engine hawa watu WA ziwani eti kwa kuwa maji Yao ni mepesi tofauti na maji ya bahari kwa kuwa mazito ......ina ukweli wowote WA hiki tunachoaminishana watu WA ziwani?
Maji ya ziwani au mto (fresh water) ni mepesi kuliko ya Bahari, lakini sio kigezo Cha wao kutumia outboard engine hata huku baharini Kuna watu wanatumia outboard engine kwenye boti kubwa.

Sababu kubwa ni gharama za inboard na Ina mambo mengi katika kuhudumia. Outboard ni very simple kuziweka na kutoa kwenye boti.

Inboard engine inataka sehemu imara ya kufunga, mounting, marine gearbox, steering system na propeller pia itabidi awe na betri Kwa ajili ya kustart na inachukua eneo kubwa tofauti na outboard.

Outboard engine ni very simple nyuma ya boti utaweka sehemu ya kufunga injini na itaelea nje haichukui nafasi. Pia injini unawasha Kwa kuvuta kamba ingawa baadhi Zina electric starting system,injini yake inamfumo wa direct cooling, gearbox na propeller zimeunganishwa pamoja katika injini sehemu ya usukani(steering) ni pale juu kwenye ule mkono ndio panatumika, hapa kitu kimoja kinakuwa kimekamilika na kinafanya kazi kama inboard engine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…