Kwema wakuu..... leo sina hamu kabisa yani, yani leo nimechezewa na Alphard kama mtoto hadi roho imeniuma sana na hadi hapa nilipo nina hasira sana na hata usingizi umegoma kabisa. Mie nilikuwa na Nissan XTRAIL old model T30.
Na ilikuwa ni msafara mmoja wa harusi na aliekuwa ananichezea ni kaka yangu na huwa hafati mziki wangu hata kidogo na hata yeye anajua hilo na kabla ya safari kuanza aliniomba nisikimbie sana. Tumetoka Singida na kwenda kuoa Mwanza, na gari zilikuwa 8 yaani Alphard 2, Nissan XTRAIL 2, IST 1, Toyota Camry 1, Kluger 1 na bus kubwa tulikodi kwa ajili ya akina mama.
Na sababu ya kuchezewa ni hii gari yani ikifika 150kph - 160kph inapandisha sana Temperature kwa hiyo inabidi upunguze hadi 100kph - 90kph ndio angalau inashusha temperature. Hii gari niliazima kwa jamaa yangu na kumuachia gari yangu Subaru Forester XT kwa kigezo cha kusave pesa kwenye masuala ya mafuta. Lakini baada ya kusave mafuta mwishowe imeniletea fedheha tu. Ila Kiukwel nimezichukia sana Nissan XTRAIL.