Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Ndani muhuni hasikii chochote😂😂😂 wa nje unaona tairi zinacheza tu, ndio maana ma VX yanawatupaga vibaya sometimes.
 
Hao wala sijiumizi, namuacha aende. Kwanza hata mafuta hanunui anaweka tu bure!
 
Nimeshangaa sana kuona kaichukulia poa D4D binafsi nimeitumia sana kwa masaa matatu dar to tanga na masaa sita Sirari to singida.
Kutoka Sirari hadi njia panda kwenda Tarime ni 25km tu,kutoka pale hadi Makutano pana kama 83km hivi,then kuitafuta Bunda pana 69km,nmesahau umbali wa Bunda hadi Lamadi junction ya kwenda Bariadi,ila toka pale hadi Mwigumbi Shinyanga ni 173 kama sijakosea,toka Mwigumbi hadi Shinyanga ni kama 40km hv, then Shy to Igunga pale mpakani nj 186km,kuimalizia Singida ni 116km

Kwa muda wa masaa sita kama ni mchana kuna uwezekano umetupiga na kitu kizito kichwani mkuu.
Hata kama ni usiku pia bado umetubonda mkuu
 
Ungekuwa na odo yenye mpaka 260, average ingekuwa tofauti sana.
I don't think so, in the real world, average isingekuwa tofauti sana. Vijiji, junctions, miji, other traffic, matuta, mataa e.t.c ni equalizers wa average.

Distance ni kilomita 208.
@180kmph utapata 69 minutes
@240kmph utapata 52 minutes

Tofauti ni dkk 17 tu ukitembea max top speed mwanzo mwisho.

Kama changamoto za road zinafanya anayetembelea 180 atumie 124 minutes instead of 69, anayetembelea 240 atatumia dakika ngapi, kumbuka kwamba kwenye hizi changamoto wote lazima washushe speed mpaka 30kmph na mwenye 240kmph anachukua muda zaidi kuifikia hiyo top speed.

Kwa hiyo difference ya dkk 17 at the end mwenye 240 atatumia 107 minutes na kupata 116kmph wakati wa 180 ametumia 124minutes na kupata 100kmph.

Difference ni 16kmph in a perfect world, na much lesser in reality. Je hiyo ni tofauti kubwa?
 
Hao wala sijiumizi, namuacha aende. Kwanza hata mafuta hanunui anaweka tu bure!
Sijajua kama ni kweli, ila nahisi migari mikubwa yenye CC kubwa haili nafuta kama vidogo dogo viwapo mbio , nahisi kagari kadogo kama IST ili kakimbie inabidi ukunje goti hadi mwisho wakati gari kama crown uki palce kidogo tu upo 120
 
Sirari singida ni km 660 sasa unashangaa kutumia masaa 6 tena usiku kwa D4D
Tazama hapo max speed ni 160.
 
Attachments

  • Screenshot_2022-08-04-20-25-52-532_com.discipleskies.android.speedometer.jpg
    132.1 KB · Views: 13
Sijajua kama ni kweli, ila nahisi migari mikubwa yenye CC kubwa haili nafuta kama vidogo dogo viwapo mbio , nahisi kagari kadogo kama IST ili kakimbie inabidi ukunje goti hadi mwisho wakati gari kama crown uki palce kidogo tu upo 120
Gari za serikali/kitengo mafuta wanawekewa ndio maana anatembea 180+ bila shida. Ukishavuka 160+ hata V8 inakunywa wese, nishatembea sana na Y62 V8 lina kiu balaa. Sasa kama V8 anatembea 170-180 wewe ili uende nae sambamba rpm muda mwingi itakuwa kwenye 4 na zaidi.
 
Sirari singida ni km 660 sasa unashangaa kutumia masaa 6 tena usiku kwa D4D
Tazama hapo max speed ni 160.

Ni sahihi kabisa usemalo, mimi kwa gari hiyo niliyokuwa nikitumia masaa matatu tanga dar mafuta naweka full ambayo inakuja 80 ltr na sitoboi katikati ya mjini bunju lazima niweke 20 ltr na ukitembea 80 kph unatumia nusu tank dar to tanga.
 
Sirari singida ni km 660 sasa unashangaa kutumia masaa 6 tena usiku kwa D4D
Tazama hapo max speed ni 160.
Mkuu max yako 160kph, avarage yako 70kph umecover vipi 660km kwa masaa 6? Gage yako ingeonesha average speed 110kph na trust me max speed ingekuwa 180kph hata mara moja.
NB: Nimetumia data za picha uliotuma.
 
Hao wala sijiumizi, namuacha aende. Kwanza hata mafuta hanunui anaweka tu bure!
Nikikutana naye pengine namuacha ila sio barabara ya Chalinze - Dar haswa usiku wa manane. Last trip natoka Dom niko Chalinze mdo mdo naovateki nashangaa anakuja ananiflashia high beams as if nimemwekea kiwingu. Tuliikaanga lami pale nikitoa katoa, nilimpoteza kuanzia kibaha kwa mathias sikumuona tena kwenye kioo mpaka mbezi nimeshusha abiria na kugeuza nikapishana naye anashuka.
 
0-180kph na engine yako cc3500 na body weight 1.5T unaweza kushinda. Na barabara nyingi zinaruhusu 0-180 max maeneo mengi. Kwahio unaweza kuwa na uwezo zaidi.
 
Mkuu max yako 160kph, avarage yako 70kph umecover vipi 660km kwa masaa 6? Gage yako ingeonesha average speed 110kph na trust me max speed ingekuwa 180kph hata mara moja.
NB: Nimetumia data za picha uliotuma.
Hiyo 160 ndio top bahati mbaya wakati na screen shot hiyo nilikuwa speed hiyo unayoiona ya 89 na muda mrefu ninapokuwa mwendo wa zaidi ya 140 kwanza siwezi kuwa na kitu natazama pembeni au kushika simu na ku screen shot.
 
Sijajua kama ni kweli, ila nahisi migari mikubwa yenye CC kubwa haili nafuta kama vidogo dogo viwapo mbio , nahisi kagari kadogo kama IST ili kakimbie inabidi ukunje goti hadi mwisho wakati gari kama crown uki palce kidogo tu upo 120
Wa diesel hachomi kama wewe mwenye petrol😂 japo at start unaweza kumfua ila high end torque ya diesel lazma iku show.
 
0-180kph na engine yako cc3500 na body weight 1.5T unaweza kushinda. Na barabara nyingi zinaruhusu 0-180 max maeneo mengi. Kwahio unaweza kuwa na uwezo zaidi.
Na barabara ya chalinze muda wote iko busy so hana muda wa kufika 200+

Plus off the line, tukitoka nyuma ya lori mimi na yeye, hichi kidude kinachomoka slightly faster. Kwahiyo kama kanitangulia namkata pale anapoovateki lori maana siwezi kumkata akishachochea labda aniachie. Then nikishakata lori nyingine 5 mbele kwa timing inakuwa game over
 
Hiyo 160 ndio top bahati mbaya wakati na screen shot hiyo nilikuwa speed hiyo unayoiona ya 89 na muda mrefu ninapokuwa mwendo wa zaidi ya 140 kwanza siwezi kuwa na kitu natazama pembeni au kushika simu na ku screen shot.
Kwamba hatujui average speed ni nini?

Au ni wewe hujamuelewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…