Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wewe kama bro wangu.
Akichoka hasikilizi yeyote.
Anasema hapa napita njia ninayoona inafaa,nyie endeleeni tu kuongea.
Haiwezekani alishapita huku,anajitokeza mtu anasema ungepita kule.
 
Wadada tumekukosea nini jamani.
Wanaume ndio wanaoongoza kwa kutoa maelekezo kwa dereva.
Kuna ajali ilitokea huku kisarawe Costa ya abiria kisarawe-machinga complex kale kasiti kadogo alikaaa mama mmoja kushoto jamaa kulia kama kawaida dereva.

Gari ikafeli breki mlimani wakati wanashuka waliogundua alikuwa huyo mama na dereva na jamaa wa kushoto mbelee..
Yule mama akapaniki akaanza kupiga kelele na kutaka ashike steering sababu ilikuwa mlimani alafu kuna Kona kalii.....
Kelele zake zikafanya abiria wa nyuma wajue gari imeshafeli mabreki abiria wengine wakapaniki nao bahati mbaya Ile gari.
Dereva alishindwa kui-controll sababu yule mama aliiing'ang'ania na huwezi amini gari Zima alikufa huyo mama TU mara nyingi wanaume Huwaga kimya ata utembee vipi ila wanagugumia ndani Kwa ndani nna shuhuda za ajali nyingi chanzo ni kelele na kupanic kwenu.
 
Alishikaje sasa usukani?🥺
 
Wakuu wa Road trip nani alishakutana na Msafara wa wale jamaa wa B.O.T?

Ilinikuta juzi kati, jamaa hawatembei sana na hawakuruhusu ku overtake.

Wanagari lao lina spika kabisa ukiwakaribia wanakutahadharisha kutoku overtake na usikae karibu.

Ni balaa
 
Mm wamenikuta mara mbili.

Mara ya Kwanza kibaha walimpasua dereva WA daladala. Unajua daladala wanavyo simama wakiwa wanashusha na kupakia. Jamaa hawana masihara kabisaa ukiwasikia wapishe waende.

Mara ya pili bwigiri niliwapisha waende nikasimama robo saa ili waende mbali zaidi.
 
Usipende sana kuwafuata...
Pale kuliwa risasi ya kichwa ni suala la kawaida...na hakuna kesi..
 
Nimeliona juzi.

Kwenye picha halitishi kama ukiliona live.

Ni kubwa si mchezo.

Na trafiki wapo tu hapo.
 
Nimeshaongozana na misafara ya JWTZ. Hawana noma kabisa. Nimeshaongozana na gari za Ikulu ambazo Rais hayupo. Hawana noma kabisa.

Sasa hawa BOT naona ni shida. Halafu kwanini wasafirishe pesa kwa barabara? Si watumie ndege na copter?
 
Nimeshaongozana na misafara ya JWTZ. Hawana noma kabisa. Nimeshaongozana na gari za Ikulu ambazo Rais hayupo. Hawana noma kabisa.

Sasa hawa BOT naona ni shida. Halafu kwanini wasafirishe pesa kwa barabara? Si watumie ndege na copter?
Nafikiri huwa inatokea mara chache.
Siku hiyo nimekutana nao njia ya Moro to Dom!
Inabidi kuwaacha kwa muda waende, ukiamsha unawakuta tena.

Nafikiri Speed yao haizidi 100 bila shaka.
 
🤣🤣🤣 Sipati picha Daladala ilikuwaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…