Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Eti wakuu kila mtu aelezee experience yake kama tochi hazipo umekabidhiwa hii mashine vxr alafuView attachment 2391934
dar - moro ( saa moja nusu ), moro - dodoma ( masaa mawili na nusu ), dodoma-singida ( masaa mawili ), singida -shinyanga ( mawili ) , shinyanga - mwanza ( saa moja ) masaa tisa yatosha
 
Hii ilikuwa jana wakati naikaribia Lindi, kijiji kinaitwa Masasiyasasa.

Niliona sungura mweupe anakimbia kutoka upande wa kushoto avuke barabara mbele yangu. Kama ilivyo ada usiku inashauriwa tusikwepe vitu vidogo kizembe. Sikujigusa.

Aliingia hapo kwenye bumper kushoto akavunja vunja. Nimekuta na contents za utumbo zimetapakaa mlango wa kushoto.

Heri ingekuwa mazingaombwe na mimi ningeamini kwamba huwa vinatokea.
 
Impact ya sungura ilifumua tu pumper upande mmoja the rest was intact. Ila wanyama hawakuta kuniacha.

Saa 12 kamili asubuhi, nikiwa kijiji cha mwisho kuingia Masasi, mbwa alikuwa katikati ya lane ya pili ya barabara. Nikaachia mguu nikabana kwangu zaidi niendelee na mambo yangu.

Kumfikia karibu, akaamua avuke barabara kwa kucross upande nnaopita. Akaingia kwenye plate number humo akaibomoa bumper chini.

Ntanunua dashcam ya kurekodi matukio na starehe za road trips.

 
dar - moro ( saa moja nusu ), moro - dodoma ( masaa mawili na nusu ), dodoma-singida ( masaa mawili ), singida -shinyanga ( mawili ) , shinyanga - mwanza ( saa moja ) masaa tisa yatosha
Approximately 8hrs up to 9hrs apo ni sawa mkuu Kuna port mmoja ivi anamuenesha mkuu flan ana vxr lc 200 aliniambia dar mwanza 5hrs akiwasha Yale mataa ya juu ya emergency
 
Pole sana chief, safari imekuwa na majanga kweli... namtumbo to songea pia kuna mbuzi wengi sana barabarani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…