Halafu hii ya kugonga nyuma sijui niaje aisee! Kuna dada mmoja alinigonga kwa nyuma, unajua kuna ile unaona kabisa ajali inakuja soon...
Ni KM chache sana kufika ilula ukitokea Iringa mjini (hilo eneo ni lile lenye upepo mwingi kwa wale wanaoijua hiyo njia) yule dada alikua na Suzuki Swifty sasa mbele yangu kulikuwa na Lorry limepata break down mie nimesimama kupisha gari za upande wa kulia zipite ili na mimi nipite.
Namuona kwenye rear view mirror anakuja tu napiga honi na hazard juu ila ndo kwanza kafunguka ghafla nikasikia kishindo!! Ikabidi nishuke namkuta anavuja damu mdomoni na puani anatetemeka hatari[emoji1787][emoji1787]. Samahani sana kaka huku anafuta damu, nikamwambia shuka nikusogezee gari pembeni kabisa ya barabara.
Aliposhuka nikamwambia kaa chini utulie nikaiweka ile gari nje kabisa ya chaki nikacheki gari yangu nyuma wala haikuumia na kubonyea zaidi ya minor scratches kwenye bampa, gari ya yule dada hood ilipinda na pia rejeta ilikuwa inavujisha. Dada alikua kafungulia mziki mkubwa nadhani ile ilimpotezea umakini.
Kaka samahani sana mi mtumishi (nurse) nimetoka manispaa nimehamishiwa ilula ndo naenda kuripoti, nikamwambia awe makini na asiendeshe gari na kobazi kama sio mzoefu ni hatari. Basi nikaondoka zangu huku nikimwambia ajaribu kwenda mdogo mdogo hadi ilula.
So mkuu hawa wanaogonga kwa nyuma ni ajali kama ila hii mara nyingi ni uzembe wa dereva.