Weeeh sijawahi pita hiyo, nimetamaniii kama vile kesho nikiwashee...[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]
Huwa nawaza na kujiuliza, ukiacha ajali barabarani hivi ndo nimekanyaga pedeli sawa sawa nimetoka Dom alfajiri naisaka Babati kupitia Kondoa. Nahisi njiani kina mapori kadhaa..... sijui kama hiyo njia inapita magari mengi....
Itakuwaje nikipata breakdown, ambazo huwa zinatokea hata kama gari iko sawa kila kitu service tairi bin vipuri.
Ila unashangaa chombo kimezima moto haupiti halafu ni saa kumi jioni...
Keeuwiiiii ntapiga uyoweeeee.... hapo ndo napataga woga wa safari ndefu.
Hizo zote nilizopiga nilikuwa nazunguka na mikonga ya DFP.
Nakumbuka safari moja tumetoka Ifakara tunawahi Msamvu kuna mtu anaenda Dom kutoka Dar tuchukue mzigo....
Hifadhi ya Mikumi suka alikuwa anaachia gia tochi zote alikuwa anaziwashia full anapita. Tulikuja kusimamishwa karibu njia panda ya kwenda Mzumbe. Suka akawaonesha kitambulisho tukauwahi mzigo Msamvu.
I love road trips [emoji3059].