Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Moshi mpaka makambako road sio mbaya kivile makambako tu songea ndio inatakiwa umakini na ilo tako la nyani na kona sio mchezo.kama unarudia mbeya kutoka kyela kuja uyole napo umakini pia na hizi mvua usije kuingia porini

Hakuna barabara ya kutoka Mbeya kwenda Mbamba Bay kupitia Kyela...

Tako la nyani haina shida ni gari ya safari...
 
Ile sio mbaya sana wakati wa kurudi kutoka kyela kuna kona chache kule kwenye mashamba ya majani ya chai maana kutoka kule asilimia kubwa unapanda kuja mbeya labda kidogo hii kushuka kuja uyole sema ukikutana na mvua kua mpole maana barabara yenyewe sehemu hua inateleza
Nimekuelewa chief... ntazingatia .. hiyo Road sijawah pita kbsaa.. hopefully hakuna magari makubwa mengi...
 
Mkuu je nikipita Moshi the arusha then manyara then natoboa dodoma then iringa then makambako...????
Hii ndio rahisi zaidi utakuwa umepunguza km nyingi tu kuliko kuzungukia chalinze.
Moshi-Arusha-Babati-Kondoa-Dodoma-Mtera-Iringa-Mafinga-Makambako-Njombe unamalizia huko mbababay

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu je nikipita Moshi the arusha then manyara then natoboa dodoma then iringa then makambako...????

Nayo ni sawa maana hii ni fupi kidogo kwa kilometa, ingawaje sina uzoefu wa kipande cha Arusha kwenda Dodoma, bila shaka chote kina lami kwa sasa...

Route yoyote kati ya hizo mbili inabidi ukaze mguu haswa maana ni zaidi ya kilometa 1400, nyingi zaidi ya Dar - Mwanza...
 
@kiduku mpapaso ananitisha kwamba tako la nyani sio gari ya safari... hii gari imetuliaaa....

kiduku mpapaso jamaa anasema hakuna Road hiyo Watu8
Mkuu nimekuambia barabara ya njombe mpaka songea inakona tena mbaya wacha nikueleze tu ukweli ili ujue kama hujawahi kupiti hio barabara.pili kutokana gari unayoenda nao huko kama ni mtu wa mbio kuingia kwenye makorongo sio kitu ya kuuliza
 
So nikiwa mbaba bay afu sitak kupitia makambako nipite road ipi..?? Wakat wa kurud..??

Nadhani swali lako ulitaka kuuliza, ukiwa Mbamba Bay na unataka kurudi Moshi pasipo kupitia Makambako...

Njia mbadala ni ya kupita Lindi lakini hii utasafiri sana na usalama ni mdogo kwa sababu utapita pembezoni mwa Tanzania na Mozambique kipande fulani hapo Tunduru...

MbambaBay - Songea - Namtumbo - Tunduru - Masasi - Mnazi Mmoja - Lindi - Dar - Chalinze - Segera - Moshi
 
Nadhani swali lako ulitaka kuuliza, ukiwa Mbamba Bay na unataka kurudi Moshi pasipo kupitia Makambako...

Njia mbadala ni ya kupita Lindi lakini hii utasafiri sana na usalama ni mdogo kwa sababu utapita pembezoni mwa Tanzania na Mozambique kipande fulani hapo Tunduru...

MbambaBay - Songea - Namtumbo - Tunduru - Masasi - Lindi - Dar - Chalinze - Segera - Moshi
Lakini si anaweza kuvuka na meli kuja kyela
 
Nadhani swali lako ulitaka kuuliza, ukiwa Mbamba Bay na unataka kurudi Moshi pasipo kupitia Makambako...

Njia mbadala ni ya kupita Lindi lakini hii utasafiri sana na usalama ni mdogo kwa sababu utapita pembezoni mwa Tanzania na Mozambique kipande fulani hapo Tunduru...

MbambaBay - Songea - Namtumbo - Tunduru - Masasi - Lindi - Dar - Chalinze - Segera - Moshi
Duhhh aisee hiii itakuwa ndefu sana.. labda Road Trip nyingine niipange kbsaa Trip hiii.. je barabara ni full lami..????
 
Back
Top Bottom