Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

View attachment 2708211

Nilianza hapa Total Shekirango, Alhamis saa 5 usiku, sahivi nipo Lushoto.

Kuanzia Mombo hadi Lushoto pamekula sana wese langu. Huu mlima consumption inashuka sana hadi 5km/L (Live consumption) ime affect average.

Nilifika Korogwe nikaongeza Lita 6 ya 20K, (PS: Diesel Engine) mida ya saa 12 asubuhi.

View attachment 2708214

Sipeleki. Moto. Kabisa. Nipo slow.

Mkuu mazda cx-5 2.2L inakupa 5km/L + iSTOP

Ntakuwa wa mwisho kuamini hili[emoji2305]
 
Mkuu mazda cx-5 2.2L inakupa 5km/L + iSTOP

Ntakuwa wa mwisho kuamini hili[emoji2305]
Ni Mazda 6 sema same engine na CX 5. Average tokea Ubungo (nili reset) hadi Mombo ilikua 26 kpl. Nilivo anza kupanda mlima average imeshuka hadi 15kpl.

Hiyo 5kpl ilikua ni live consumption, sio average. Yaan pale unavokanyaga inakua inakuandikia kwamba this second unatumia mafuta hivi kwa lita.

Ukiwa unashuka mlima inaandika hadi 60kpl.

Nitajaribu kupiga pic nitashare.
 
Ahaaa kwa live consumption sawa

Hongeraa sana chuma kalii, enjoy skyActiv

Vp swala DPF umesolve vp mkuu,?
 
Kwa injini hiyo hiyo niliweka full tank Puma mwenge 33l nimefika nayo Arusha na kuzunguka kidogo mpaka taa imekuja kuwaka ilikua 621km.
Juzi kuamkia jana nikaweka hizo hizo zimenifikisha Dar na bado ninayo. Na hapo kati nilikilmbizana mnoo na LC 300 kwanzia mwanga mpaka mombo. Ashukuriwe huyo mwenye LC na king’ora chake T*** AQM mlinichangamsha naimani na nyinyi mlichangamka kama mpo humu japo sio kiushindani. Kwahiyo kama gari yako iko na service nzuri naimani around 60lit zina kufikisha. Jitahidi kama una uwezo sehemu kubwa ya safari yako iwe usiku. Dar-Arus-Dar nimetumia 221000. Hiyo buku nilimpq afande ya kahawa sikua na kosa nikaona nimtoe. Iliyobaki ni mafuta. Nilisimama mara chache kuchimba dawa. Niliondoka puma mwenge saa 10:47 usiku nilifika Mianzini saa 6:30 asubuhi. View attachment 2695373
Hiki kidashbod cha passo kama sio ractis 🤣 kuwa makini mkuu.
 
Ahaaa kwa live consumption sawa

Hongeraa sana chuma kalii, enjoy skyActiv

Vp swala DPF umesolve vp mkuu,?
Hapa ndio natoka Lushoto.
1000107892.jpg

Consumption ya mlimani Live hii hapa

1000107904.jpg

Lakini ikaja mteremkoni hii hapa hadi 60.
1000107908.jpg

Ila average ni 22 sahivi.

1000108056.png
 
Nimekamirisha safari

1000109805.png

Mafuta ya 240,000/= Diesel
Gari cc 2,200

Nilichojifunza:
(1) Kama unapenda kuendesha, make sure una company.
(2) Endesha sana usiku. Pametulia sana.
(3) Ukifika kwenye mji zurura na baiskeli, bajaji, boda au ya miguu gari park. Itasevu wese sana.
(4) Kunywa sana maji. Huwezi sinzia ukiwa na mkojo.
(5) Cruise control ni life saver.
(6) Speed ya 70-80 kph ndio nzuri kwa kutunza mafuta.
 
Nimekamirisha safari

View attachment 2712544

Mafuta ya 240,000/= Diesel
Gari cc 2,200

Nilichojifunza:
(1) Kama unapenda kuendesha, make sure una company.
(2) Endesha sana usiku. Pametulia sana.
(3) Ukifika kwenye mji zurura na baiskeli, bajaji, boda au ya miguu gari park. Itasevu wese sana.
(4) Kunywa sana maji. Huwezi sinzia ukiwa na mkojo.
(5) Cruise control ni life saver.
(6) Speed ya 70-80 kph ndio nzuri kwa kutunza mafuta.

Yangu November ntachukua ushauri

Dsm-Moshi-kahama -mwanza-Dsm
 
Wazee mpo! Leo Nina trip ndefu sana. Tayari nimeanza mda huu kutokea Ubungo kuelekea Bukoba.

Nitawapatieni updates. Sala zenu wakuu

Update:

Saa5:03 Msamvu. Hapa nina notification moja ya ku overtake, nurse amegoma kula buku2 akaandika.
 
Back
Top Bottom