Creative Monster
Member
- Jul 22, 2019
- 10
- 27
Creative Monster
Baraza la wazee liliwahi kuomba vijana wawe na heshima kwa wazee hususani kwenye daladala pale wazee wanapokosa viti basi vijana wasimame kuwapisha wazee wakae. Ni kweli na ni swala zuri sana na la kuenzi.
Septemba mosi ndani ya daladala iliyokuwa ikitokea Mbagala kuelekea Mawasiliano, babu mmoja ambaye jina lake halikufahamika alilazimika kumpisha kijana mdogo kwenye kiti akae huku yeye akisimama na abiria wengine waliokuwa wamekosa viti. Mzee huyo alidai alishatumia nafasi yake ujajani ila hakujiongeza kununua gari lake mwenyewe mpaka anazeeka.
Watu wengi walistaajabu kwanini mzee yule mwenye umri wa kuheshimika na kila mmoja aliyekuwemo kwenye daladala kuanzia abiria, dereva mpaha kondakta kumuachia kiti mwanafunzi huku watu kadhaa wakijaribu kumuachia kiti kingine lakini hakuhitaji tena kwamba anajipa adhabu ya kusimama kwa uchungu wa kushindwa kufanikiwa akiwa kijana.
Mzee yule alizungumza kwa uchungu mkubwa sana huku akiwataka vijana kujituma na kuacha starehe kwani ndicho kitu kilichomponza yeye. Kwa mujibu wa maelezo yake, aliwahi kufanya kazi kwenye kiwanda kimoja kikubwa Dar es salaam (jina limehifadhiwa) akapata cheo kikubwa na uhakika wa mshahara mkubwa na marupurupu kibao. Lakini pamoja na hao yote uzee wake hauna mafao hata kidogo kwa maana alitumia vibaya pesa hadi madaraka hadi kupelekea kuharibu kazi wakati ambao alikuwa ameshasogea kiumri bila mafanikio yoyote.
Mbali na hayo mzee hakutaka huruma kwa kile alichodai kuwa ni ishara ya kudharaulika maana mpaka unafikia hatua ya kuonewa huruma kuna vitu huwezi au hustahili kwahiyo ni fedheha kubwa mno.
Nilichojifunza kwa babu huyo (mzee) kwenye daladala ya Mbagala kwenda Simu200 (Mawasiliano)
Alikuwa ni mzee wa makamo, lakini alilazimika kuachia kiti ili mvulana mwanafunzi mwenye makamo ya miaka 16 hivi akae. Mzee alikuwa na sababu zake chache tu za kwanini ampishe kijana mdodo kwenye kiti?
i/. Kijana alikuwa anaenda shule
Katika daladala nyingi sana wanafunzi wananyanyasika kwa sababu nauli yao ni shilingi 200, basi wanazuiwa wasikae na endapo kuna abiria wengi wasiosoma basi kondakta anashusha wanafunzi ili apige pesa, kwahiyo mzee alimpisha kijana ili afike shuleni bila uchovu akasome kutimiza ndoto zake na baadae apande gari lake na siyo daladala tena.
ii/. Mzee alishatumia muda wake wa kupanda daladala
Kwa mujibu wa mzee yule ni kwamba hata yeye alikuwa kijana, hivyo alishindwa kutumia ujana wake kufanikisha ndoto ya wengi ya kumiliki nyumba na gari kwahiyo anaona kusimama kwenye gari ni adhabu anayojipa kwa kutumia vibaya fursa alizozipata wakati wa ujana wake.
iii/. Ujana ni maji ya moto
Nafasi ya kuwa kijana ipo moja tu, ikishapita imepita hivyo kuna vitu ukiwa unavifanya lazima uwaze mbele hasa katika siku zijazo za uzee wako kuwa utaishi katika hali gani. Mfano: pale unapotumia pesa unazopata kwa ajili ya anasa baadaye yako itakuwa haina mafao na matokeo yake utajikuta ukifanya safari zako kwa miguu, na wakati mwingine huna pa kuishi au anasumbuliwa na magonjwa kwa matumizi ya vilevi wakati wa ujana.
iv/. Maisha ya uzee ni zao la ujana/epuka fedheha uzeeni
Licha ya kuwa waatu wengi wametoka kwenye familia zenye uwezo lakini eneo la UJANA huwa linawaacha vibaya pale wanaposhindwa kulitumia. Wengine huishia kufungwa kwa matumizi ya vilevi ikiwemo bangi na madawa ya kulevya. Wazee wengi unaowaona mtaani wakichoma mahindi, wakiuza maji, mbogamboga au kuombaomba, siyo wote walikosa fursa au kukutwa na janga asilia ujanani au ulemavu, wengine walitumia vibaya walichokipata. Imefikia wakati hawana namna wameamua kujiajiri kwenye hizo kazi ili wasiishie kukosa kabisa kwa maana walishindwa kudumisha msingi wakati wa ujana.
v/. Heshima ni haki lakini pale unapostahili, kuhurumiwa ni kudharaulika
Kondakta mmoja pale mawasiliano alimshusha mzee kwenye daladala akimwambia kuwa hawezi kumudu kusimama kwa maana watu walijaa sana, hii ilichagizwa na mwonekano wa mzee yule kuwa na afya isiyoimara na hata hivyo hakuonekana kuwa mzee wa kisasa. Mara nyingi wazee wa kisasa wakipanda kwenye daladala kwanza huwa wanaonekana kuwa wamepanda kwa bahati mbaya pengine gari limeharibika au kuna kitu cha ziada sana. hawa mara nyingi huachiwa kiti kwa kuheshimiwa na siyo kuhurumiwa.
Katika kuhakikisha unajenga kesho nzuri, ni lazima leo yako iwe katika maandalizi ya ugeni mkubwa wa kesho yako.
Wazee wetu tunawapenda sana, tunawaheshimu na kuwathamini mno. Lakini hali wanayomaliza nayo hasa kwenye uchumi aidha na magonjwa inatufundisha tufanye nini tukiwa vijana. Tujiburudishe kwa anasa za pombe, sigara na starehe za wanawake/wanaume bila mpangilio?- matokeo yake ni magonjwa na kutumia vibaya rasrimali pesa. Tuwekeze kwenye biashara, kilimo na ufugaji. Pengine tufungue miradi binafsi kwa ubunifu. Tuendelee kuwapenda wazee wetu na kuacha kuwatuhumu vibaya na vitendo vya ushirikina pamoja na kuwafanyia vitendo vya kikatili.
Sayansi ina mchango gani katika kutengeneza kesho bora?
a/. Kufanya biashara kwenye mitandao ya kijamii na wakati mwingine kutumia mitandao kutafuta wateja kwa kutangaza bidhaa zako.
b/. Miundombinu imeboreshwa sana kuanzia vitendea kazi vya kisasa zaidi na mazingira ya masoko ili kurahisisha uuzaji wa bidhaa/mazao. Barabara, reli, bandari na usafiri wa anga ni mazao ya sayansi na teknolojia hivyo yanatumika vizuri kusafirishia bidhaa kitaifa na kimataifa.
c/. Elimu; kila kitu kinapatikana kwenye mtandao, hata vitu vya kijinga vinapatikana pia lakini mtandao ukiutumia vizuri utajifunza sana maisha ikiwemo namna ya kufanya vitu mbali mbali, ufugaji, kilimo au ubunifu na sanaa.
Kuna nafasi moja tu ya kuishi, epuka fedheha uzeeni.
NI BORA UPANDE DALADALA UKIJUA MAMBO YAKO SALAMA, KULIKO KUPANDA DALADALA KWA KUWA HAKUNA NAMNA NYINGINE.
HESHIMA SIYO KUHURUMIWA, NA KUHURUMIWA NI SEHEMU YA KUDHARAULIKA. VIJANA TUJENGE MAISHA YA KESHO

Upvote
5