informer 06
Member
- May 11, 2024
- 66
- 49
Waziri wa Afya,Jenista Mhagama amezitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhari ya magonjwa ya msimu ambayo yamekuwa yakiibuka kwa nyakati tofauti hususani ugonjwa wa kipindupindu ambao amedai umekuwa ukipelekea vifo.
Amesema kuwa ugonjwa wa Kipindupindu umekuwa ukiwachukuwa watu. Lakini ameeleza kwamba ugonjwa huo umekuwa ukisabishwa na uchafu.
Akizungumza leo January 3, 2025 akiwa katika hospitali ya Mkoa wa Kagera iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Mhagama ameyataja magonjwa mengine kama Corona, Ugonjwa wa virusi vya Marburg pamoja na mengine.
Katika kuchukua hatua za kukabiliana na athari za magonjwa hayo amesema kwamba Serikali ipo katika mpango wa ujenzi wa hospitali maalumu mkoani Kagera kwa ajili ya magonjwa ya mlipuko.
"Pamoja na jambo la maalumu la wahudumu wa afya ngazi ya jamii lakini mimefanya kazi kukagua mpango wa Serikali, azima ya Serikali, nia ya Serikali ya kuwa na Hospitali maalumu kwa ajili ya magonjwa ya mlipuko katika Mkoa wetu wa Kagera"amesema
Lakini amebainisha jitihada nyingine kwamba ni kutoa nguvu kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii ambao wanaendelea kupatiwa mafuzo kwa ajili ya kuanza kuhudumia jamii, amesema kuwa wahudumu hao wataenda kuongeza nguvu ya katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya ambazo zinakumba jamii.
Aidha amesema kwamba wahudumu hao wanajengewa uwezo wa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kushauri, kufanya vipimo kwa baadhi magonjwa pamoja na kubaini viashiria vya magonjwa na kuchukua hatua stahiki mapema.
Licha ya hivyo amewahasa wahudumu kuzingatia miiko ya kazi ikiwemo kutunza siri za watu wanaowahudumia, ambapo amesisitiza kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaoenda kinyume na miiko ikiwemo suala hilo la kutunza siri.